Friday, January 25, 2019

VITUO VYA WATOTO YATIMA VYAPOKEA MSAADA WA CHAKULA.




    Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie ametoa misaada ya vyakula vyenye thamani ya sh. 3,120,000 (milioni tatu laki moja na elfu ishirini) kwa vituo viwili vya watoto yatima siku ya leo.
   Misaada hiyo imekabidhiwa asubuhi ya leo kwa niaba ya Nabii Mkuu nae Mngojezi wa Nabii Mkuu, Bw. Abiud Luila kwa wasimamizi wa vituo vya Faraja Orphanage center, Bw. Faraja, pamoja na kwa msimamizi wa kituo cha Christian Woman Orphanage Care anayeitwa Mchungaji Zakia Hatib.
   Vitu vilivyotolewa ni pamoja na mchele kg. 600 wenye thamani ya sh. 1,320,000 (milioni moja, laki tatu na elfu ishirini), mafuta ya kupikia lita 300 yenye thamani ya sh. 1,200,000 (milioni moja na laki mbili) pamoja na sukari kg. 240 yenye thamani ya sh. 600,000 (laki sita).
   Wakizungumza baada ya kupokea misaada, wasimamizi wa vituo hivyo wametoa shukurani zao za dhati kwa Nabii Mkuu kwa upendo wake pamoja na moyo wa kusaidia alionao kwa watu wote bila kujali dhehebu, dini wala kabila.
   Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie amekuwa na kawaida ya kutoa misaada mbalimbali katika vituo vya watoto yatima kila mwanzo wa mwaka ambapo zoezi hilo litaendelea kwa vituo vingine.

NB: Usisahau kudownload application ya GeorDavie Ministries itakayo kuwezesha kutazama  GeorDavie Tv pamoja na kusikiliza 99.3 N.Y.U Radio




Pichani ni Mngojezi wa Nabii Mkuu, Bw. Abiud Luila (kushoto) akikabidhi misaada kwa niaba ya Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie,  kwa msimamizi wa kituo cha Faraja Orphanage.
Baadhi ya vitu vilivyotolewa kama misaada katika vituo vya watoto yatıma.

Baadhi ya vitu vilivyotolewa katika  vituo vya watoto yatima.

Baadhi ya vyakula vilivyotolewa kwa watoto yatima.

Katika picha ni Mngojezi wa Nabii Mkuu, Bw. Abiud Luila (kushoto) katika picha ya pamoja na Msimamizi wa kituo cha Christian Woman Orphanage Care, wakati akimkabidhi misaada kwa niaba ya Nabii Mkuu Mhe. Dr. GeorDavie.

No comments:

Post a Comment