Kisiwani Mafia Tanzania, Mafuta ya
petrol na dizeli huuzwa kwa reja reja katika vibanda, huku kukiwa hakuna
sheli ya mafuta kwa ajili ya mahitaji ya matumizi ya watu wenye vyombo
vya usafiri kisiwani humo.
Ofisi
ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira imesema changamoto iliyopo
katika kupata taarifa sahihi za Wazanzibar wanaopata ajira katika
Taasisi za Muungano anuani ya makazi.
Rwanda imetangaza
mpango wa ushirikiano na timu ya Arsenal inayocheza ligi kuu ya
England.Ushirikiano huo wa miaka 3 unalenga kuimarisha sekta ya utalii
nchini Rwanda,uwekezaji na maendeleo ya mchezo wa soka.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustine Mahiga
amesema Watanzania waishio nje ya nchi wanatuma zaidi ya Sh trilioni
moja nchini kwa mwaka.
NAIBU
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto dkt. Faustine
Ndugulile amethibitisha kuwa hakuna mtu aliyethibitika kuwa na ugonjwa
wa EBOLA hapa nchini wala hakuna ugonjwa huo hapa Tanzania.
Maofisa
watatu wa Kituo cha Uwekezaji cha nchini (Tanzania Investment Center
(TIC) wamefariki dunia katika ajali ya gari usiku wa kuamkia jana Mei
22, 2018 maeneo ya Chalinze wakiwa njiani kuelekea jijini Dodoma.
Mbunge
wa Muleba Kusini(CCM), Profesa Anna Tibaijuka ameitaka serikali ya
awamu ya tano iwajibike kuwanunulia ng'ombe wafugaji walioshinda kesi
zao Mahakamani kama sheria inavyosema nasio vinginevyo.
Rais wa Marekani Donald Trump ametoa
matamshi yanayokinzana na ya mshauri wake wa masuala ya usalama wa
taifa, akisema mfumo wa Libya wa kumaliza zana za nyuklia hauwezi
kutumiwa nchini Korea Kaskazini.
Rais
wa Marekani, Donald Trump amepinga kauli ya mshauri wake mkuu wa
masuala ya ulinzi, John Bolton aliyedai kuwa mfumo wa kuondoa silaha za
kinyuklia nchini Korea Kaskazini utafanana na uliotumika Libya.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
amempongeza mwanamitindo wa kimataifa Bibi. Flaviana Matata kwa juhudi
za kusaidia watoto wa kike kupata elimu kwa kuwawezesha vifaa muhimu
vya shule ikiwemo ada na madaftari.
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania(TFF) limewaondoa Waamuzi wawili kwenye orodha ya Waamuzi wa
Ligi ya Mabingwa wa Mikoa(RCL) inayoendelea kwenye vituo vinne vya
Geita,Singida,Rukwa na Kilimanjaro.
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai
(kushoto) akisalimiana na mgeni wake Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Nchi
za Ukanda wa Maziwa Mkuu Mhe. Onyango kakoba (kulia) alipomtembelea leo
Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,
ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM), amepewa tuzo
ya heshima na klabu ya soka ya Coastal Union ya jijini Tanga.
Kiongozi
wa China Xi Jinping ndiye mtu mwenye ushawishi Zaidi duniani, kwa
mujibu wa jarida la Forbes. Amechukua nafasi hiyo baada ya bunge China
kumpa mamlaka zaidi na kuondoa kikomo cha muhula wa rais.
Waziri mkuu wa zamani wa Malaysia
Dr.Mahathir Mohamad amepata ushindi wa kihistoria katika uchaguzi mkuu
uliofanyika katika hilo. Kiongozi huyo ameweza kukiangusha chama ambacho
kimekuwa madarakani tangu mwaka 1957 ambacho kimekuwa kikidaiwa
kujihusisha na nasuala ya rushwa na ufisadi.
Nashindwa hata niongelee vipi neno
tatizo.Sababu kila mmoja ana maana yake.Na matatizo yanatofautiana
kutoka kwa mtu hadi mtu.Familia hadi familia,ukoo hadi ukoo,jamii hadi
jamii.na taifa hadi taifa.
Katika kuongeza mapato kwenye Halmashauri ya Wilaya ya
Arusha na kupunguza malalamiko ya wananchi ya kulalamikia kuibiwa pindi
wanapolipa bili ya maji serikali ya halmashauri hio chini ya Shirika
lisilo la kiselikari lijulikanalo kwajina la Water aid limeunda mfumo
mpya wa upatikanaji wa maji ujulikanao kwa jina la e water ambao
utadhibiti mianya ya ukwepaji kodi
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph
Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga
wakilakiwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mh. Freeman Mbowe mara baada ya
kuachiwa huru leo Alhamis Mei 10,2018 jijini Mbeya.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger
alipoteza fursa pekee ya kushinda kombe msimu wake wa mwisho akiwa
katika klabu hiyo baada ya kuchapwa na Atletico Madrid katika nusu
fainali ya ligi ndogo ya klabu Ulaya Europa League.
Mkuu
wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara amepewa onyo
kali na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kutoka na yeye kuingia uwanjani
kushangilia ushindi wa timu yake mara baada ya kumalizika kwa mchezo
kati ya Simba na Yanga uliochezwa Aprili 29, 2018.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako,
amewajia juu baadhi ya watumishi wa serikali ambao wanatabia ya
kuwafukuza kazi walimu wakuu wa shule ambao hutoa matokeo mabaya katika
mitihani ya Taifa.
Naibu
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ametoa wito
kwa wabunge kutojihusisha na vitendo vya kingono na wafunzi wa vyuo
vikuu na wawaache wasome.
Serikali
imeagiza wakuu wa mikoa, wilaya na maofisa biashara kufuatilia na
kuwachukulia hatua wafanyabiashara wanaopandisha bei ya sukari kwa
makusudi katika kipindi hiki cha kuelekea mwezi wa mfungo wa Ramadhani.
Mamlaka
ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), juzi ilitangaza
kushuka kwa bei ya petroli na dizeli kwa asilimia 2.7 na asilimia 3.8;
na ongezeko la asilimia 0.09 kwa mafuta ya taa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema
kuwa tangu aingie madarakani wameajiri jumla ya watumishi 18,101 katika
sekta mbalimbali nchini.
Akizungumza leo Mei 1 mkoa Iringa katika siku ya Wafanyakazi ambapo amesema jumla ya watumishi 22,150 wanatarajia kuwaajiri.
Mshambuliaji
wa Taifa Stars na Klabu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta amewaonya
vijana wa timu ya taifa ya mpira wa miguu waliochini ya miaka 17,
Serengeti Boys kwa kuwataka waache kubweteka kufuatia ushindi wa kombe
la CECAFA mwaka 2018.
Waziri
wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine
Mahiga ameomba radhi kwa Rais Magufuli kwa niaba ya watu wa Iringa kwa
kukosa kura 25 kipindi cha kampeni za uchaguzi mwaka 2015.