Monday, October 23, 2023

MKUU WA WILAYA YA ARUMERU AMPONGEZA NABII MKUU KWA KUSAIDIA JAMII

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Emmanuela Mtatifikolo Kaganda amempongeza Nabii Mkuu Mhe. Dkt. GeorDavie kwa kazi anayoifanya katika kuisadia jamii kiroho na kijamii.

Ametoa pongezi hizo alipokuwa akizungumza katika ibada ya chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika nyumba ya matamko ngurumo ya upako ambapo ilikuwa ni ibada ya Adhimisho la zawadi ya Nabii Mkuu.

Akizungumza katika ibada hiyo amemuomba Nabii Mkuu kuendelea kuwasaidia watu kiroho na hata kijamii huku akisema kuwa ameguswa na jambo ambalo Nabii Mkuu amelifanya la kuwasapoti wanawake waliokuwa wanajiuza.

Na Beatrice Maina, N.Y.U ARUSHA.

No comments:

Post a Comment