Monday, October 30, 2023

NABII MKUU DKT. GEORDAVIE "HEKIMA NA UFAHAMU NI CHANZO CHA KUMJUA MTAKATIFU WA MUNGU"

Nabii Mkuu Mheshimiwa Dkt.GeorDavie amesema kuwa mtu anaweza kuwa na hekima lakini akakosa ufahamu.

Nabii Mkuu ameyasema hayo alipokuwa akifundisha katika ibada ya chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika nyumba ya matamko ngurumo ya upako kisongo Arusha ambapo ilikuwa ni iabada ya kupokea hekima na ufahamu.

Akifundisha kuhusu somo lililokuwa na kichwa kisemacho kumjua mtakatifu ni ufahamu Nabii Mkuu amesema kuwa kumjua aliyechaguliwa na Mungu, kumjua mteule aliyebeba kusudi la wakati au majira ni ufahamu.

Pia Nabii Mkuu ameitangaza wiki hii kuwa ni wiki ya kupokea hekima na ufahamu.

Na Beatrice Maina.



No comments:

Post a Comment