Monday, October 23, 2023

NABII MKUU ATOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 27 KUSAIDIA WATU MBALIMBALI WAKIWEMO WANAWAKE WALIOKUWA WANAJIUZA.

Nabii Mkuu Mhe. Dkt.GeorDavie Balozi wa Amani jumapili ya jana ametoa fedha zaidi ya shilingi milioni 27 kusaidia watu mbalimbali wakiwemo wanawake ambao walikuwa wakijiuza ili kujiingizia kipato cha kujikimu kimaisha.

Nabii Mkuu ametoa fedha hizo katika ibada ya chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika nyumba ya amtamko ngurumo ya upako kisongo mkoani Arusha na ilikuwa ni ibada ya adhimisho la zawadi ya Nabii Mkuu.

Akizungumza wakati anatoa msaada huo kwa watu hao Nabii Mkuu amesema amewataka watu kutambua kwamba huduma ya kinabii ni huduma yenye mamlaka maana ukitamka neno linakuwa kwa sababu wanawake hao walisikia agizo na kulifuata kwa kuamua kubadilika na kuongeza kuwa kazi waliyokuwa wakiifanya ilikuwa inahitaji ufungulivu wa kiroho kabla ya kuwasapoti.

Pia Nabii mkuu ametangaza kuwa hii ni wiki ya kuepushwa na ajali na kupokea ulinzi mkamilifu.

Aidha Ibada hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Mkuu wa wilaya ya Arumeru Emmanuela Mtatifikolo Kaganda Pamoja na Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Mhe. Mrisho Gambo na watumishi wa Mungu kutoka makanisa mengine ikiwa ni Pamoja na Baraza la Mitume na Manabii Tanzania.

Na Beatrice Maina - N.Y.U ARUSHA.











No comments:

Post a Comment