Thursday, July 24, 2025

HII NDIO CV YA KOCHA MPYA WA KLABU YA YANGA.

 HII NDIO CV YA KOCHA MPYA WA KLABU YA YANGA.

Anaitwa Romain Folz (35) Kocha mpya wa Yanga,ambae alizaliwa Bordeaux,Ufaransa πŸ‡«πŸ‡·

Huyu kocha amefanya kazi sehemu zifuatazoπŸ‘‡

2025 Alikuwa Mkurugenzi wa michezo wa Olympique Akbou ya Algeria πŸ‡©πŸ‡Ώ

2024 Alikuwa kocha msaidizi wa Mamelodi Sundown ya South Africa πŸ‡ΏπŸ‡¦

2023 Alikuwa kocha mkuu wa Horoya ya Guinea πŸ‡¬πŸ‡³

2022 Alikuwa kocha mkuu wa Amazulu ya South Africa πŸ‡ΏπŸ‡¦

2021 Alikuwa kocha Mkuu wa Township Rollers ya Botswana πŸ‡§πŸ‡Ό

2019 Alikuwa kocha Msaidizi wa Pyramid ya Egypt πŸ‡ͺπŸ‡¬

2018 Alikuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Uganda πŸ‡ΊπŸ‡¬

Huyu kocha ana UEFA Pro Licence na Pro Licence ya CONMEBOL (America).

Huyu kocha ni Muhumini wa (4-3-3) na timu yake ina-press kinoma.

NABII MKUU MHE.DKT.GEORDAVIE LEO HII ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI.

Nabii Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie leo ametunukiwa shahada ya Udaktari wa heshima na tuzo ikiwa ni kumuheshimisha kutokana na mambo mengi anayofanya katika kuisadia jamii.

‎Tukio hilo limefanyika katika ukumbi wa Sephil Saphire mnamo julai 5, 2025  mjini Dodoma kuanzia majira ya saa tatu asubuhi hadi saa Saba mchana na limeandaliwa na umoja wa Chama Cha Madaktati na Maprofesa Tanzania.

Akizungumza baada ya kutunukiwa shahada hiyo ya falsafa ya udaktari Nabii Mkuu Mke. Dkt. GeorDavie amesema umempa hamasa kubwa na msisimko mpya wa kuendelea kuisaidia jamii na kushughulika na mahitaji mbalimbali ya watu katika kuleta maendeleo kwa ujumla.

‎Akizungumza mara baada ya kumtunuku shahada hiyo mgeni rasmi ambaye pia ni Mwenyekiti wa umoja wa Chama Cha Madaktati na Maprofess, Prof. Rejoice Ndalima amesema kuwa Nabii Mkuu amestahili kwa sababu amekuwa akisaidia wananchi bila kubagua.

‎Aidha tukio hilo kubwa na la kihistoria limehudhuria na Madaktati na Maprofesa wa hapa nchini, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Taifa, watumishi wa Mungu pamoja na watu kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.

Na Beatrice Maina@NYU ARUSHA.




NABII MKUU MHE.DKT GEORDAVIE ATAKA AMANI YA NCHI ILINDWE.

‎‎Nabii Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie amewataka wananchi kulinda Amani iliyopo nchini.

‎‎Nabii Mkuu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari katika ukumbi wa Sephil Saphire jijini Dodoma.

‎" Tulinde Utulivu na Amani katika Nchi ya Tanzania pia tujitoze kupiga kura kwa sababu ni swala la msingi na Haki ya Kila mtu"/Amesema Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie Balozi wa Amani Taifa.

‎Aidha amewataka pia viongozi wa Dini kuendelea kumuombea Rais na kuyasema yote mema aliyoyafanya katika kutekeleza shughuli mbalimbali ya kimaendeleo.

‎Na Beatrice Maina@NYU ARUSHA. #GeorDavietv YouTube #GeorDavietv Instagram #GeorDavie Facebook #GeorDavie TikTok #GeorDavie Maarifa







NABII MKUU MHE DKT. GEORDAVIE LEO AMETOA ZAWADI YA GARI AINA YA BMW KWA MWALIMU ISAYA BENSON.

Nabii Mkuu Mhe.Dkt.GeorDavie mchana wa Leo amemzawadia Mwalimu wa NENO la Mungu Isaya Benson Gari aina ya BMW X5 na shilingi milioni mbili kwa msikilizaji wa NYU FM RADIO kijana Makochali ambaye alizungumza jambo lililomgusa Nabii Mkuu.

‎‎Nabii Mkuu ametoa zawadi hizo mchana wa Leo kupitia kipindi cha zijue TABIA ZA MITUME NA MANABII kinachorushwa na NYU RADIO kila siku ya jumamosi kuanzia saa nne kamili asubuhi hadi saa Saba kamili mchana.

‎‎Akitoa zawadi hiyo ya gari kwa Mwalimu Isaya Nabii Mkuu amesema anampongeza kwa kazi nzuri anayofanya ikiwemo kipindi cha Maswali na Majibu, Tabia za Mitume na Manabii na kipindi cha Hazina katika Historia huku akimuelezea Mwalimu Isaya kuwa ni kijana mchapa kazi ,anayefanya tafiti mbalimbali na anaeleza kiustarabu.

‎‎Kwa upande wake Mwalimu Isaya Benson amemshukuru Nabii Mkuu kwa kumpandisha thamani kwa mara nyingine kwa kumpa BMW X5.

‎‎Aidha mpaka muda huu ambapo habari hii inakwenda hewani bado Nabii Mkuu anaendelea na zoezi la utoaji wa zawadi kwa wasikilizaji ambao wanapata nafasi ya kupiga simu studio za NYU RADIO na kuulizwa maswali kisha kuzawadiwa shilingi elfu hamsini(50) kwa kila mtu ambapo hadi sasa watu 10 tayari wamejipatia zawadi hizo.

‎Na Beatrice Maina @NYU ARUSHA. #GeorDavietv YouTube #GeorDavietv Instagram #GeorDavie Facebook #GeorDavie TikTok #GeorDavie Maarifa