Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 26 Juni, 2016 amefanya mabadiliko
Sunday, June 26, 2016
Ugonjwa Usiofahamika Ulioibuka mkoani Dodoma Na Kuwaathiri watu 32 Wafahamika
WAZIRI
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu,
amesema ugonjwa usiofahamika ulioibuka mkoani Dodoma, unatokana na
sumukuvu inayopatikana kwenye nafaka.
Akizungumza
jijini, Dar es Salaam jana, Ummy alitolea ufafanuzi kuhusu ugonjwa huo
na kuongeza ndani ya wiki moja, kumekuwa na ongezeko la wagonjwa 11 na
kufanya jumla ya wagonjwa kufikia 32, ingawa idadi ya vifo
haijaongezeka.
Alisema
majibu kuhusu ugonjwa huo yanatokana na uchunguzi wa awali uliofanywa
na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) na kwamba serikali imechukua
nafaka kadhaa zinazopatikana mkoani Dodoma ili kuzipeleka Atlanta,
Marekani kwa uchunguzi zaidi.
“Tulitoa
taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa huo Juni 19 mwaka huu ambao ulipatikana
wilaya za Chemba na Kondoa, kulikokuwa na wagonjwa 21 na vifo saba, hata
hivyo mpaka kufikia juzi wagonjwa waliokumbwa na ugonjwa huo
wameongezeka na kufikia 32 na idadi ya vifo imebakia saba,” alisema Ummy.
Alisema
katika jitihada za kutambua kiini cha ugonjwa huo, Wizara imepeleka
jopo la wataalamu huko Dodoma ili waweze kushirikiana na wenzao walioko
huko kufanya uchunguzi wa kina wa ugonjwa huo.
Alisema
sampuli mbalimbali za damu, haja ndogo, haja kubwa, vinyama vya ini na
sampuli za vyakula, zilipelekwa katika maabara za Mkemia Mkuu wa
Serikali, maabara ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Maabara ya Taifa
ya Magonjwa ya Binadamu na maabara ya Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya
Moshi mkoani Kilimanjaro.
“Vile
vile sampuli nyingine kesho zitapelekwa Marekani katika maabara ya
Kituo cha Udhibiti wa Magonjwa cha Marekani (CDC) kilichopo Atlanta kwa
uchunguzi zaidi,” alisema Ummy.
Aidha alisema, “kuna
uwezekano mkubwa kwamba ugonjwa huu umesababishwa na ulaji wa chakula
kilichokuwa na sumukuvu na kuleta madhara, ili kuwa na uhakika na jambo
hilo Wizara yangu inasubiri matokeo ya vipimo vya damu na haja ndogo
vilivyopelekwa katika Maabara ya CDC matarajio yetu ni kupata majibu
hayo katika kipindi kisichozidi wiki moja.”
Alisema tangu ugonjwa huo ulipoibuka, wagonjwa 12 wametibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na 18 wametibiwa Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.
Alisema tangu ugonjwa huo ulipoibuka, wagonjwa 12 wametibiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na 18 wametibiwa Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.
Tuesday, June 21, 2016
Bemba ahukumiwa miaka 18 jela
Aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini
Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Jean-Pierre Bemba, amehukumiwa kifungo cha
miaka 18 jela kufuatia uamuzi wa mahakama ya kimataifa ICC, kutokana na
uhalifu wa kivita na unyanyasaji wa kingono.
Analaumiwa kwa kushindwa kuwazuia waasi wake wasiwaue na kuwabaka watu. Mawakili wa Bemba tayari wamesema kuwa watakataa faa kupinga hukumu hiyo.
Akitoa hukumu hiyo jaji Sylvia Steiner, alisema kuwa Bemba alishindwa kudhibiti waasi wake ambao walitumwa kwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati.
wafuasi wa bwana Bemba wakifuatilia hukumu yake kutokea DRC
Bemba alikuwa ametuma zaidi ya wapiganaji 1,000 kwenda nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kumsaidia rais wa zamani Ange Felix Patasse, kukubiliana na jaribio la mapinduzi.
BREAKING NEWS: GHASIA MBAYA ZASHUHUDIWA AFRIKA YA KUSINI
Polisi nchini Afrika Kusini wanajaribu kuzua ghasia ambazo zimetokea maeneo ya mji mkuu wa nchi hiyo Pretoria.
Taarifa
ya serikali ambayo inataka kuwepo utulivu, inasema kuwa maafisa wa
polisi walifyatuliwa risasi wakati waandamanaji waliposhambulia gari lao
kwa mawe.Ghasia zilianza katika eneo la Tshwane kutokana na suala la mgombea wa kiti cha meya ambaye aliteuliwa na chama cha ANC kugombea uchaguzi mwezi Agosti.
Vyombo vya habari nchini humo vinaonyesha vizuizi vinavyowaka moto.
Serikali ya Afrika Kusini imeoamba kufanyika kwa mazungumzo ili kusuluhisha tatizo hilo.
WABUNGE UPINZANI WAENDELEA KUGOMEA VIKAO VYA BUNGE, LEO WATOKA KIMYAKIMYA
Wabunge
wa Ukawa wameendelea kususia vikao vinavyoongozwa na Dk Tulia Ackson,
lakini leo wametoka kimyakimya bila mbwembwe kama za jana.
Kwa sasa kamati ya uongozi ya umoja huo imeingia kufanya kikao kujadili mustakabali wao.
Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema watatoa taarifa kamili baada ya kumaliza kikao hicho.
Tuesday, April 26, 2016
RAIS MAGUFULI AMEIVUNJA BODI YA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA)
Rais Magufuli ameivunja Bodi ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dkt. Ally Yahaya Simbakutokana na
Monday, April 25, 2016
Friday, February 5, 2016
SERIKALI YABAINISHA VIKWAZO VYA MAENDELEO YA TAIFA
Serikali
Imesema tatizo la ukuajiwa uchumi usioenda na maisha halisi ya mtanzani
umechangiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kasi kubwa ya
Monday, February 1, 2016
IBADA YA JPILI TAR 31 JANUARY 2016
Wito umetolewa kwa Wanangurumo kudumisha moyo wa utoaji kwani
hakuna ufalme wa mungu hauwezi kuendelea pasipo wana wa
Friday, January 29, 2016
Tuesday, January 26, 2016
BUNGE LA 11 MKUTANO WA PILI UMEANZA RASMI MJINI DODOMA
Bunge la 11 mkutano wa pili kikao cha kwanza la Jamhuri ya
muungano wa Tanzania limeanza leo mjini Dodoma ambapo limefunguliwa kwa
Subscribe to:
Posts (Atom)