Ligi kuu ya soka ya England
inaendelea tena wikendi hii kwa michezo kadhaa,kesho jumamosi michezo
saba inatarajiwa kuchezwa ambapo Liverpool wanacheza na Stoke
city,Burnley dhidi ya Brighton,Crystal Palace ni mwenyeji wa Leceister
City.
Kim Jong-un amekuwa kiongozi wa
kwanza wa Korea Kaskazini kuingia Korea Kusini kwa kuvuka mstari wa
kijeshi uliowekwa kugawanya mataifa hayo mawili tangu vita vya Korea
1953.
Katika hatua ilioshangiliwa kwa mbwembwe za kila aina
kiongozi wa Korea Kusini na mwenzake wa Korea Kaskazini walisalimiana
kwa mikono katika mpaka huo.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha
kukamatwa kwa watu 9 waliokuwa wakiandamana eneo la Samora Avenue,
Posta.
Mchezo wa nusu fainali ya pili UEFA Champions Leag, mkondo
wa kwabza kati ya Bayern Munichen dhidi ya Real Madrid, ulipigwa usiku
wa kuamkia leo huko Allianzi Arena huku Madrid wakiibuka wababe katika
mchezo huo.
Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum Jijini Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, ametolea
ufafanuzi suala ambalo limeanza kushika hatamu mitandaoni la kukamatwa
kwa Katibu wa Baraza la Wanawake CHADEMA kata ya Kisutu Elizabeth
Mambosho na kupelekwa rumande akiwa na mtoto mchanga.
Hali
ni shwari mkoani Manyara. Hakuna dalili za maandamano. Hata hivyo
askari polisi wakiwa na magari, pikipiki na kutembelea kwa miguu
walionekana wakizunguka sehemu mbalimbali ili kuimarisha ulinzi.
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewataka wananchi wote
kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa kuwa maandamano
yanayozungumzwa hayapo na ni batili.
Watu tisa wameuawa mjini Toronto,
nchini Canada baada kugongwa na gari la mizigo ambalo lilielekea katika
mtaa wenye watu wengi. Wengine 16 wamejeruhiwa pia.
Mashuhuda wanasema kuwa dereva huyo aliendelea kuliendesha gari takribani umbali wa kilomita moja hivi.
Serikali
imesema treni inayotumia umeme inatarajiwa kuanza kutoa huduma Novemba
mwakani kwa usafiri wa reli ya kati, kipande cha Dar es Salaam -
Morogoro.
Mkuu
wa mkoa wa Dar es salam Paul Makonda jana April 9 amezungumza na akina
mama waliotelekezwa na waume zao jijini Dar es Salaam ambapo mamia ya
wanawake hao wamejitokeza wakiwa na watoto zao.
Nyumba
12 zilizopo kando ya Mto Msimbazi,Mtaa Majengo Eneo la Vingunguti
jijini Dsm zimesombwa na Maji na huku nyingine zaidi ya 100 ziko
hatarini kuanguka kutokana na Mmomonyoko wa Udongo unatokana na kupanuka
kwa Mto Msimbazi na kuingia katika makazi ya watu.
Tanzania
inakadiriwa kuwa na wafungwa 40,000 wakati uwezo wa magereza yake ni
30,000 hivyo kuna ongezeko la zaidi ya wafungwa 10,000 katika msongamano
huo.
MMILIKI wa lori Mitsubishi Fuso
lililogongana na basi la City Boys katikati ya wiki iliyopita na
kusababisha vifo vya watu 12 hapa wilayani Igunga mkoani Tabora,
amekamatwa na polisi mkoani Ruvuma.
Wanachama
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza, wanakusudia kufanya
maandamano ya amani Aprili 26, mwaka huu, kuunga mkono na kupongeza kazi
kubwa inayofanywa na Rais Dkt John Pombe Magufuli
Mamlaka
katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali imetangaza kuanza msako mkali na
kuwaweka gerezani walemavu wote wanaojihusisha na vitendo vya kuomba
omba barabarani, kwa madai kuwa ni chanzo cha uchafu wa jiji hilo.
Vyombo
vya habari nchini Syria zimeripoti vifo vya watu kadha katika uwanja
mmoja wa Ndege wa kijeshi nchini humo baada ya shambulio la kutumia
Makombora.
Mbunge
wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Godbless Lema hajasita kuweka wazi hisia zake baada ya kutambulishwa na
RC Gambo katika Ibada ya kusimikwa Mhashamu Isaack Amani kuwa Askofu
Mkuu Jimbo la Katoliki la Arusha.
UONGOZI wa Jeshi la China umeahidi kuisaidia na kuiunga mkono Urusi kijeshi kukabiliana na mataifa ya Magharibi dhidi ya mzozo wa kidiplomasia, vikwazo vya kiuchumi na mazoezi ya kijeshi.
Ahadi hiyo imetolewa Waziri wa Ulinzi wa China, Wei Feng ambaye yuko Urusi
Luis Suarez amefunga goli lake la
kwanza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupita karibu mwaka
mmoja wakati Barcelona ikiifunga Roma magoli 4-0 katika mchezo wao wa
kwanza wa robo fainali.
Liverpool imejiweka vyema katika
Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupata matokeo mazuri kwa robo
fainali kwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Manchester City
yaliyopatikana ndani ya dakika 31 za kwanza katika dimba la Anfield.
Mahakama
ya Wilaya ya Dodoma leo Aprili 5, 2018 imepokea taarifa ya vipimo vya
kitabibu vya Tito Machibya (Nabii Tito) ili kujua kama ana matatizo ya
akili au la.
Majambazi
wamevamia Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto
Yesu-Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam na kupora fedha na baadhi ya
vifaa vya kuendeshea misa usiku wa kuamkia leo.
Watu
12 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia ajari ya basi
la kampuni ya City bus lililogana uso kwa uso na fuso katika kijiji cha
makomelo wilayani Nzega mkoani TABORA.
Chelsea wanatarajia kumteua kocha wa
Juventus, Massimiliano Allegri, kuwa meneja wa mpya mwishoni mwa msimu
lakini kama itashindikana mazungumzo na meneja wa zamani wa Barcelona
Luis Enrique. (Star)
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wanafunz wa Kidato
cha Sita kutoka shule 11 za Mkoa huo wakati wa ufunguzi wa Kambi ya
Kitaaluma kwa wanafunzi hao Aprili 03 wilayani Maswa.
Taasisi ya Utafiti Repoa imetoa
tahadhari ikisema licha ya juhudi zinazoendelea katika mageuzi ya
kiuchumi, Serikali inapaswa kushughulikia vikwazo vilivyopo ili
kukabiliana na ushindani wa masoko nje ya nchi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi Ijumaa hii Aprili 06, 2018 kwenye uzinduzi
wa ukuta kwenye migodi ya Mirerani mkoani Arusha.