Saturday, October 28, 2023

NABII MKUU MHE. DKT. GEORDAVIE JUMAPILI YA KESHO ATAONGOZA IBADA YA CHUO KIKUU CHA MANABII

Nabii Mkuu Mhe. Dkt. GeorDavie jumapili hii anatarajia kuongoza ibada ya chuo kikuu Cha manabii ambapo itakuwa ni ibada ya kupokea hekima na ufahamu.

Akizungumza kuhusu ibada hiyo Nabii Mkuu amesema kuwa pia itakuwa ni siku ya kuwasilisha sadaka za International Partner kwa ajili ya ununuzi wa viti.

Amesema kuwa katika ibada hiyo ya kupokea hekima na ufahamu neno la linalosimamia ni kutoka katika kitabu cha Mithali 9:10 unaosema "Kumcha Bwana ni mwanzo wa hekima na kumjua mtakatifu ni ufahamu"

Aidha Nabii Mkuu amemtaka kila mtu kuwahi ibadani,kuja na sadaka ya international partner pamoja na sadaka maalum ya kupokea hekima na ufahamu.

Na Beatrice Maina, N.Y.U ARUSHA.


Monday, October 23, 2023

MKUU WA WILAYA YA ARUMERU AMPONGEZA NABII MKUU KWA KUSAIDIA JAMII

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Emmanuela Mtatifikolo Kaganda amempongeza Nabii Mkuu Mhe. Dkt. GeorDavie kwa kazi anayoifanya katika kuisadia jamii kiroho na kijamii.

Ametoa pongezi hizo alipokuwa akizungumza katika ibada ya chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika nyumba ya matamko ngurumo ya upako ambapo ilikuwa ni ibada ya Adhimisho la zawadi ya Nabii Mkuu.

Akizungumza katika ibada hiyo amemuomba Nabii Mkuu kuendelea kuwasaidia watu kiroho na hata kijamii huku akisema kuwa ameguswa na jambo ambalo Nabii Mkuu amelifanya la kuwasapoti wanawake waliokuwa wanajiuza.

Na Beatrice Maina, N.Y.U ARUSHA.

NABII MKUU ATOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 27 KUSAIDIA WATU MBALIMBALI WAKIWEMO WANAWAKE WALIOKUWA WANAJIUZA.

Nabii Mkuu Mhe. Dkt.GeorDavie Balozi wa Amani jumapili ya jana ametoa fedha zaidi ya shilingi milioni 27 kusaidia watu mbalimbali wakiwemo wanawake ambao walikuwa wakijiuza ili kujiingizia kipato cha kujikimu kimaisha.

Nabii Mkuu ametoa fedha hizo katika ibada ya chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika nyumba ya amtamko ngurumo ya upako kisongo mkoani Arusha na ilikuwa ni ibada ya adhimisho la zawadi ya Nabii Mkuu.

Akizungumza wakati anatoa msaada huo kwa watu hao Nabii Mkuu amesema amewataka watu kutambua kwamba huduma ya kinabii ni huduma yenye mamlaka maana ukitamka neno linakuwa kwa sababu wanawake hao walisikia agizo na kulifuata kwa kuamua kubadilika na kuongeza kuwa kazi waliyokuwa wakiifanya ilikuwa inahitaji ufungulivu wa kiroho kabla ya kuwasapoti.

Pia Nabii mkuu ametangaza kuwa hii ni wiki ya kuepushwa na ajali na kupokea ulinzi mkamilifu.

Aidha Ibada hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Mkuu wa wilaya ya Arumeru Emmanuela Mtatifikolo Kaganda Pamoja na Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Mhe. Mrisho Gambo na watumishi wa Mungu kutoka makanisa mengine ikiwa ni Pamoja na Baraza la Mitume na Manabii Tanzania.

Na Beatrice Maina - N.Y.U ARUSHA.











MRISHO GAMBO "KAZI ANAZOFANYA NABII MKUU ZINAIONYESHA KUWA NI DINI YA KWELI"

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe. Mrisho Gambo amesema kwamba kazi anazozifanya Nabii Mkuu Mhe. Dkt. GeorDavie katika kuwasaidia watu kiuchumi ni ishara tosha kuwa hiyo ndio dini ya kweli.

Mhe. Gambo ameyasema hayo alipokuwa akitoa zawadi kwa Nabii Mkuu Mkuu Mhe. Dkt. GeorDavie ambapo ilikuwa ni sikukuu ya adhimisho la zawadi ya Nabii Mkuu.

Aidha amesema kuwa amekuwa akijifunza mambo mengi wakati wote anaposhiriki ibada za huduma ya ngurumo ya upako kwani ipo tofauti na huduma nyingine.

Na Beatrice Maina, N.Y.U ARUSHA






PICHA ZA SHAMRASHAMRA ZA WATU NA MATUKIO MBALIMBALI WAKATI WA KUMPOKEA NABII MKUU MHE. DKT. GEORDAVIE KATIKA NYUMBA YA MATAMKO.















NABII MKUU MHE. DKT. GEORDAVIE "HII NI WIKI YA KUEPUSHWA NA AJALI NA KUPOKEA ULINZI"

Nabii Mkuu Mhe. Dkt. GeorDavie ametangaza neno la wiki hii kuwa hii ni wiki ya kuepushwa na Ajali na kupokea Ulinzi mkamilifu.

Ametangaza neno hilo jumapili ya Oktoba 22, 2023 katika ibada ya chuo kikuu cha manabii iliyofanyika katika nyumba ya matamko kisongo Arusha ambapo ilikuwa ni ibada ya kupokea Thawabu ya Nabii Mkuu na ilikuwa ni sikukuu ya adhimisho la zawadi ya Nabii Mkuu.

Nabii Mkuu Mhe. Dkt. GeorDavie amesema kuwa neno la kinabii linapokuja limekusudiwa kuwakinga wana wa Mungu na mabaya yote ya adui.


Sunday, November 17, 2019

#NENO LA WIKI HII KINABII LATANGAZWA/NABII MKUU KUWEPO TENA JUMAPILI IJAYO/WAGENI HAWA KUHUDHURIA

NABII MKUU TANZANIA MH DKT GEORDAVIE AMETANGAZA KUWA HII NI WIKI YA MAWAZO YAKO KUPATA KIBALI,

NABII MKUU AMETANGAZA NENO HILO HII LEO KATIKA IBADA YA CHUO KIKUU CHA MANABII HEMANI KISONGO ARUSHA AMBAPO ILIKUWA NI IBADA YA KUPATANISHWA NA MADHABAHU.

NA NABII MKUU AMESEMA HIVI