Bingwa wa uzani mzito duniani Deontay Wilder anadai kwamba amekubali kuzipiga dhidi ya Anthony Joshua nchini Uingereza
Raia huyo wa Marekani mwenye umri wa miaka 32 anashikilia taji la WBC na anataka pigano la kuunganisha mataji hayo na Anthony Joshua anayeshikilia mataji matatu ya WBA, IBF na bingwa wa WBO.
Alituma ujumbe wa Twitter: Ombi la kupigana nami la $50m nchini Marekani pia lipo. Leo nimekubali kupigana na Anthony Joshua nchini Uingereza.
Promota wa Joshua, Eddie Hearn aliambia Sky Sports atatuma hati za kandarasi hiyo lakini hajui iwapo madai hayo ya Wilder yana ukweli wowote.
Aliongezea: Tumeshangazwa na Deontay Wilder kurudi kwetu na ombi hilo na inaonekana kwamba amekubali masharti yake.
''Kitu kimoja ambacho nitakwambia ni kwamba mwisho wa wiki hii , Deontay Wilder atapokea kandarasi hii na tutajua iwapo ni mkweli''.
Hearn amekuwa akiikosoa timu ya Wilder kwa kuamua kufanya kazi zao kupitia mitandao ya kijamii akisisitiza kuwa mikataba huafikiwa katika chumba cha mazungumzo na wala sio katika instagram.
"Iwapo atapendelea pigano hilo kufanyika Uingereza basi ni wao wa kuamua ,aliongezea Wilder.
Meneja wa Wilder Shell Finkel aliambia EPSN kwamba wamekubali masharti kupigana nchini Uingereza.
Alisema: Deontay alituma ujumbe kwa Joshua siku ya Jumapili na mimi nikatuma mwengine siku ya Jumatatu kwa Barry Hearn na Edie nikiwaambia kwamba tumekubali rasmi ombi hilo kupigana chini ya masharti waliotupatia na tukawaambia watutumie kandarasi.
Iwapao Joshua 28, atapigana na bondia huyo wa Marekani, mshindi atakuwa bondia wa kwanza wa uzani mzito duniani kushikilia mataji manne duniani kwa wakati mmoja.
Bondia wa Urusi Alexander Povetkin anataka kuwania taji la WBA na anakaribia kupigana na Joshua , ijapokuwa Joshua huenda akapambana na Wilder iwapo Povetkin ataweza kupigana na mshindi.
No comments:
Post a Comment