Rais
Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wamemaliza
mazungumzo ya kwanza ya kihistoria kwa kutia saini taarifa juu ya ahadi
za kuangamiza silaha za nuklia za Korea Kaskaizni.
Trump akizungumza baada ya kutia saini hati hiyo amesema ameridhika kabisa na mazungumzo na wameanzisha uhusiano mzuri kati yao.
"Ninadhani
uhusiano kamili kati yetu na Korea Kaskazini utabadilika na kua tofauti
na namna ilivyo kua awali na tumeweza kukuza uhusiano mzuri kuliko vile
tulivyotarajia."
Akiulizwa ikiwa atamualika Kim Washington alijibu, Bila shaka.
Kim kwa upande wake amesema wamekubaliana kuacha nyuma yaliyopita na kufungua ukurasa mpya wa uhusiano.
Kabla
ya kutia saini Trump na Kim walikutana kwa mara ya kwanza na kupeana
mkono asubuhi katika hoteli ya Capella kwenye kisiwa cha mapumziko cha
Sentosa, huko Singapore.
Baadae
tena wakakutana ana kwa ana kwa karibu dakika 40, kabla ya kutoka na
kukutana pamoja na wajumbe wao wa vyeo vya juu. Katika mkutano huo
kulikuwepo mawaziri wa mambo ya nchi za nje na wakuu wa usalama wa taifa
wa kila upande.
Walipomaliza
mazungumzo hayo viongozi hao walikula chakula cha mchana wakiendelea na
mazungumzo bila yakufahamika kile walichokua wanazungumza.
No comments:
Post a Comment