Tuesday, June 12, 2018

Vifo vyaongezeka Ajali ya wanafunzi UDSM


Majeruhi mmoja kati ya wawili wa ajali iliyotokea eneo la River Side jijini Dar es Salaam ikihusisha gari la wagonjwa la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amefariki dunia leo Juni 12, 2018.

Majeruhi huyo alikuwa akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (Moi) baada ya ajali iliyotokea usiku wa jana Juni 11, 2018.

Ofisa uhusiano wa Moi, Patrick Mvungi amesema waliwapokea majeruhi hao saa 9:30 usiku wakitokea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

Amewataja majeruhi hao kuwa ni Abishai Nkiku (24), mwanafunzi wa UDSM na Jonathan Lugando (40), mhudumu wa chuo hicho.

Amesema Lugando aliyeumia zaidi kichwani amefariki dunia asubuhi.

Mvungi amesema Nkiku ameumia kichwani na amevunjika mkono wa kushoto.

"Madaktari wanaendelea kumhudumia Nkiku ingawa ameumia sana kichwani,” amesema Mvungi.

No comments:

Post a Comment