Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wazi kuwa suala la kutangaza
nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma hadharani husababisha
athari kwa jamii nzima na kwa wale ambao siyo watumishi.
Hayo
yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiwa bungeni kwenye
kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge
Suzani Lyimo aliyehoji ni kwa nini serikali ya awamu ya tano inakiuka
sheria ya utumishi wa umma ya kutoa nyongeza kwa watumishi wake.
Mh.
Majaliwa amesema kwamba siyo kwamba serikali haikusudii kuongeza
mshahara kwa watumishi wake lakini kutumia siku kama Mei 1 kutangaza
nyongeza za mishahara husababisha athari kwa wananchi wote kwani vitu
vinaweza kupanda bei na kusababisha usumbufu kwa watu wengine wasiopokea
mishahara.
Pamoja
na hayo, Mh Majaliwa ameeleza kuwa "Suala la mshahara ni siri ya mtu.
Siyo lazima litangazwe hadharani. Ndiyo maana hata tunapolipa madeni
hatutangazi lakini wanaodai wanaona kwenye mishahara yao kwamba malipo
yanaingia. Lengo la serikali ni kupunguza na gharama za maisha".
Ameongeza
"Serikali ina utaratibu wa kuwapa stahiki watumishi kadiri inavyotakiwa
na inaratibiwa vizuri. Tunaendelea na uboreshaji wa maeneo hayo kama
nyongeza za mshahara, na upandishaji wa wa madaja. Watumishi wawe na
imani na serikali. Rais alitenga zaidi ya bilioni 200 na tumeshaanza
kulipa madeni. Nyongeza za mishahara zitatolewa kwani Rais alikwisha
ahidi"
No comments:
Post a Comment