Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako Ndalichako
ameweka wazi kwamba serikali haiwezi kuvumilia vitendo vya
udhalilishaji ambavyo vimeonekana kufanywa na mwalimu wa shule St.
Florence iliyopo jijini Dar es salaam.
Waziri
Ndalichakoameyasema hayo wakati akikabidhi zawadi kwa shule na
wanafunzi wa darasa la saba, kidato cha nne na sita jijini Dodoma baada
ya kufanya vizuri kwenye matokeo ya mwisho ya mitihani yao.
Akizungumzia
suala hilo Ndalichako amewahakikishia wananchi kuwa mwalimu
aliyewafanyia udhalilishaji wanafunzi wa kike wa shule ya Mt. Florence
vyombo vya dola vinaendelea na uchunguzi lakini watahakikisha serikali
inawamchukulia hatua kali.
Pamoja
na hayo Waziri Ndalichako ameshauri walimu wa kike kusafiri na
wanafunzi wa jinsia ya kike katika ziara mbalimbali za kishule badala ya
wanaume ili kuepukana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kama
ilivyowatokea wanafunzi wa shule St. Florence.
Hivi
karibuni kuliibuka sintofahamu ndani ya jiji la Dar es salaam na
Tanzania kwa ujumla baada ya kuwepo na taarifa kwamba katika shule ya
St. Florence mwalimu mmoja aliyetajwa kwa jina la Ayubu kudaiwa
kuwanajisi watoto wanne wa darasa la saba.
No comments:
Post a Comment