Monday, July 22, 2019

Filamu ya ‘The Lion King’ imeingia kwenye rekodi hii ya mauzoSHARE


Leo July 22,2019 filamu ya The Lion King imechukua headlines baada ya kutajwa kuwa mpaka sasa imefanikiwa kuingiza kiasi cha zaidi ya shilingi Trilioni 1 za Kitanzania duniani kote tokea iachiwe rasmi July 19,2019.

Filamu hiyo imetajwa kushika rekodi na kuingia kwenye list ya filamu yenye mauzo makubwa katika kipindi cha uzinduzi wa filamu za kutazamwa chini ya kampuni ya PG Film na katika soko la Amerika ya Kaskazini imefanikiwa kuigiza kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 426 za Kitanzania.

Hili ni toleo la pili la Filamu ya ‘The Lion King’ ambapo toleo la kwanza lilikuwa la katuni (Animation) la mwaka 1994 ikiwa pia toleo hili jipya limeshirikisha sauti za mastaa mbalimbali akiwemo Beyonce Knowles (Nala), Donald Glover(Simba), John Oliver(Zazu) na wengine weng
i

No comments:

Post a Comment