HOSPITALI
ya rufaa ya Haydom Wilayani Mbulu, Mkoani Manyara imenunua mashine mpya
ya kisasa ya uchunguzi (X-ray) kwa lengo la kuhudumia wagonjwa wengi,
kuongeza ufanisi na kutoa huduma kwa urahisi zaidi.
Hospitali
hiyo inahudumia wagonjwa wa zaidi ya mikoa sita nchini, ikiwemo
Manyara, Singida, Dodoma, Tabora, Arusha na Simiyu ambapo kifaa hicho
kitaongeza mikakati ya kupandishwa hadhi kuwa hospitali ya kanda.
Mkurugenzi
wa hospitali ya Haydom Dk Emmanuel Nuwass alisema mashine hiyo mpya ya
kisasa ya kidigital imenunuliwa kwa gharama ya shilingi milioni 30.
Dk
Nuwass alisema mashine hiyo ya kisasa kutoka Ufaransa itasababisha
ufanisi mkubwa katika utendaji kazi wake katika kuwahudumia wagonjwa wa
hospitali hiyo tofauti na awali.
Alisema
mashine hiyo ina uwezo mkubwa wa kupiga picha kwa ubora na muda mfupi
tofauti na ile iliyokuwa inatumika kwa teknolojia ambayo imepitwa na
wakati.
"Mashine
hii ni ya kisasa na ya kipekee kwani kwa hapa nchini zipo mbili za
toleo hili katika hospitali ya Haydom na hospitali ya Bugando jijini
Mwanza," alisema Dk Nuwass.
Alisema
mashine hiyo ya kisasa ya mionzi zaidi ya kuhudumia watu wengi kwa muda
mfupi, ubora wa picha zake utasababisha tatizo la mgonjwa kuonekana kwa
urahisi.
Alisema
pamoja na kutoa huduma kwa wagonjwa pia mashine hiyo itaongeza mikakati
yao ya kufanikisha hospitali hiyo kupandishwa hadhi kutoka ya rufaa
hadi kuwa ya kanda.
Hata
hivyo, mmoja kati ya wakazi wa eneo hilo, John Matle aliyekuwa
hospitalini hapo alipongeza jitihada za Dk Nuwass katika kuboresha
miundombinu ya hospitali ya Haydom.
"Ile
mikakati ya kuhakikisha hospitali ya rufaa ya Haydom inakuwa ya kanda
inaweza ikafanyika kutokana na mikakati na mipango bora kama hii
inayofanywa na Dk Nuwass," alisema Matle.
Mkurugenzi
wa hospitali ya rufaa ya Haydom Mkoani Manyara, Dkt Emmanuel Nuwass
akiwaangalia mafundi wakifunga mashine mpya ya kisasa ya X-Ray ya
thamani ya shilingi milioni 300.
Mafundi
wakiendelea kufunga mashine mpya ya kisasa ya hospitali ya rufaa ya
Haydom Mkoani Manyara, wakiendelea kushoto ni Mkurugenzi wa hospitaki
hiyo Dkt Emmanuel Nuwass.
BY RICH VOICE.
No comments:
Post a Comment