Wednesday, July 3, 2019

NUNDU APIGA HESABU ZA UBUNGE JIMBO LA TANGA 2020

ALIYEKUWA Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano katika serikali ya awamu ya nne Mhandisi Omari Nundu ametangaza nia ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Tanga mwaka 2020 mara baada ya kipenga kutangazwa rasmi. 
Mhandisi Nundu alitangaza nia hiyo wakati wa halfa ya kukabidhiwa vifaa vya Hospitali ya wilaya ya Tanga vilivyotolewa na wadau wa maendeleo mkoani Tanga kupitia magroup ya mitandao ya kijamii ya Whatsup. 

Alisema kwamba wakati ukifika wa kuchukua fomu atafanya hivyo kwa kuchukua na kujaza ikiwemo kuirudisha ili kuwa tayari kwa ajili ya kinyang’anyiro hicho ili kuomba ridhaa ya wananchi wamchague ili awatumikie. 
Mhandisi Nundu ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) kwa kipindi cha miaka mitano kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 kubwagwa na mgombea kutoka Chama cha Wananchi (CUF) Alhaji Mussa Mbaruku. 
“Labda niwaambie kwamba ikifika mwaka 2020 wakati wa kugombea nitachukua fomu nitazijaza na kugombea lakini kwa sasa hamtoniona nikigawa fedha kwa watu elfu ishirikiniishirini wala futari “Alisema Waziri huyo wa zamani 
“Nimesikia maneno mtaani yanapita kwamba Nundu anataka kugombea ubunge niwaambie kwamba ikifika mwaka 2020 wakati wa kugombea nitachukua fomu nitaijaza na kurudisha”Alisema .Aidha alieleza kwamba hatawapa fedha watu lakini kwenye suala la maendeleo atashirikiana na wananchi kuhakikisha yanapatikana kwa kutatua baadhi ya changamoto. 
“Nitasimamia suala la maendeleo mpaka hatua ya mwisho sasa tuna Rais ambaye anasaidia na kusukuma maendeleo kwa kasi kubwa kwani matunda yake yameonekana kwenye sekta mbalimbali”Alisema 
Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji alisema kwamba niwashukuru wote waliochangia vifaa hivyo vya matumizi ya hispiotali nikiri hivi sasa tutakuwa tunapokea vifaa kwa utaratibu wa kiserikali. 
Mayeji alisema kwamba wao serikali wanapokea misaada yoyote ile hasa isiyo na masharti watapokea na wanaingiza kwenye matumizi hawana sababu yoyote ya kukataa kitu ambacho kimekuwa kikitolewa na wadau. 
Watawakabidhi wataalamu waugavi kwa ajili ya kuvipokea huku akieleza kwamba wao kama serikali hawana masharti ya kutokupokea msaada wowote ambao umekuwa ukitolewa. 
“Kama kuna mtu anahitaji kutoa msaada kwenye Jiji la Tanga tupo tayari kupokea lakini kikubwa tufuate utaratibu ambao unatakiwa kwa kupeleka kunakohusika na watapokea na kupeleka kwenye matumizi yanayokusudiwa “Alisema Mkurugenzi huyo. 
Alisema wamevipokea na vitatumika kwenye matumizi yalyokusudiwa ili viendelee kutumika kwa kuwekewa uangalizi mzuri wa matumizi.

No comments:

Post a Comment