Upandaji
holela wa miti katika njia kuu za Umeme Wilayani kahama mkoani
Shinyanga umetajwa kuchangia kusababisha Nishati hiyo kukatika mara kwa
mara kutoka na miti hiyo kugusa nyanya za Umeme.
Kauli
hiyo imetolewa na Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
wilayani Kahama Mhandisi King Fokanya wakati akizungumza na waandishii
wa habari ofini kwake kuhusiana namna walivyojipanga kutoa elimu kwa
wananchi juu ya utunzaji wa miundombinu ya umeme.
Amesema
katika maeneo mengi wilayani humu wananchi wamepanda miti mikubwa
katika karibu na nguzo za umeme jambo ambalo linaweza kuleta madhara
makubwa pindi nguzo zinapo anguka ama kuguswa na miti hiyo.
Amefafanua
kuwa pindi Shirika hilo linapotaka kuikata baadhi yao wamekuwa
wakilaumu juu ya ukataji wa miti hiyo katika njia za umeme na watumishi
wake katika oparesheni za kuhakikisha miundombinu hiyo inakuwa salama.
Katika
Hatua nyingine Mhandisi Fokanya amesema katika mwaka wa fedha wa
2019/2020 Ofisi yake imepokea shilingi milioni 847 kwa ajili ya kupeleka
huduma ya nishati ya umeme kwenye kata 10 ambazo hazina umeme zilizopo
Halmashauri ya Mji wa Kahama na Msalala.
Amefafanua
kuwa shilingi Milioni 847 zimegawanya katika makundi mawili ambapo
shilingi milioni 402 zitatumika kupeleka huduma ya nishati ya umeme
kwenye kata 10 msalala na kahama mjini huku Milioni 445 zinatumika
kwenye mategenezo ya kubadilisha nguzo,vikombe, maboresho ya Transfoma
na vifaa vilivyoharibika.
Kata
ambazo zinapelekewa huduma hiyo ni pamoja kata ya Muhungula, Nyakato,
Mbulu, Mhongolo, Nyashimbi, Nyihogo sekondari, Kagongwa, Mwendakulima
Isaka na Kakola.
by rich voice
No comments:
Post a Comment