Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na
Waziri wa Habari, Utalii na Mambo Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit
Kombo na Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ally Abeid
Karume wamesaini makubaliano ya ushirikiano katika kusimamia na
kutekeleza sekta za Habari, Utamaduni,Sanaa na michezo ili kuongeza
tija.
Uwekaji
wa saini za ushirikiano huo umefanyika jana Jijini Dodoma katika ukumbi
wa chuo cha Ufundi Veta, baada ya vikao vya ngazi za wataalam na
Makatibu Wakuu wa Wizara husika kuwasilisha taarifa hizo kwa Mawaziri na
hatimaye kuridhia tayari kwa ajili ya utekelezaji.
“Hatua
hii ni nzuri na muhimu kwetu katika kuhakikisha tunadumisha na
kuhifadhi muungano wa kihistoria ambao ulioasisiwa na waasisi wa Taifa
hili Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere na Shehe Amani Abed Karume”
Alisisitiza Dkt. Mwakyembe.
Aidha,
Waziri wa Habari, Utalii na Mambo Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit
Kombo ameeleza kuwa katika sekta ya habari ni muhimu kwa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) kushirikiana na Shirika la Utangazaji
Zanzibar (ZBC) ili kuandaa vipindi mbalimbali ikiwemo kipindi cha
utalii Safari chaneli.
“Kwa
kutambua umuhimu wa sekta ya utalii nchini , vyombo hivi vya habari
TBC na ZBC vinapaswa kushirikiana kuandaa vipindi vya utalii ili
kuitangaza sekta hii nje na ndani ya nchi” Alisisitiza Mhe. Mahmoud
Thabit Kombo .
Kwa
upande wake Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ally
Abeid Karume amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili
inatangazwa na kuenezwa kuna umuhimu wa kuandaa kanzi data
itakayojumuisha wataalam wa Kiswahili ambao watakuwa wakifundisha
wageni ndani na nje ya nchi.
“Tanzania
imechangia sana katika kukuza lugha ya Kiswahili na watu wengi
wanapenda kuja kujifunza kwetu ,hivyo naamini kwa kuwa na kanzi data hii
itasaidia sana katika kuwapata watalaam wazuri wa kufundisha lugha
hii”. Balozi Ally Abeid Karume.
Vilevile
Mawaziri hao wamekubaliana kuimarisha ushirikano katika sekya ya sanaa
kwa kuhakikisha kuwa ifikapo desemba 2019 wanakuwa wamesha andaa kanuni
zitakazowawezesha watayarisha wa filamu kutoka nje ya nchi ili kuruhusu
utumiaji wa maudhui hayo kwa vyombo vya habari vya serikali.
Mawaziri
hao walimalizia kwa kueleza kuwa sekta ya michezo ni sekta muhimu sana
katika kutambulisha taifa kupitia michezo mbalimbali na hivyo
walikubaliana kuandaa kombe la Muungano, namna bora ya kuibua na
kukuza vipaji pamoja na kuteua wajumbe wa bodi ya Baraza laTaifa la
Michezo (BMT) na Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar.
Vilevile
Mawaziri hao walipata wasaa wa kutembelea shule ya Fountain Gate
Academy iliyopo maili mbili Jijini Dodoma, ambayo huibua na kuendeleza
vipaji vya michezo kwa vijana wenye vipaji hivyo ili kuwaendeleza na
kuweza kufikia ndoto zao ikiwa ni moja ya jitihada za kuendeleza sekta
ya michezo nchini.
No comments:
Post a Comment