Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan, ameshiriki katika Mkutano wa 12 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na
Serikali wa Umoja wa Afrika kuhusu Mkataba wa Uanzishwaji wa Eneo Huru
la Biashara la Afrika (AfCFTA) unaofanyika jijini Niamey nchini Niger.
Makamu
wa Rais Mhe. Samia ameipongeza Serikali ya Ghana kwa kuchaguliwa kuwa
Makao Makuu ya Sekretarieti ya AfCFTA na kuisihi Kamisheni ya Umoja wa
Afrika kuharakisha ukamilishaji wa muundo, wa bajeti na mpango kazi wa
Sekretarieti hiyo ili ianze kufanya kazi haraka.
Mkutano
huo wa Wakuu wa nchi na Serikali umepokea taarifa ya Mheshimiwa
Mahamadou Issoufou, Rais wa Jamhuri ya Niger kuhusu utekelezaji wa
AfCFTA ambayo imepokelewa na kupishwa na viongozi hao. Mkataba wa
Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) umeanza kazi
rasmi tarehe 30 Mei, 2019 na unahusu uasili wa bidhaa zitakazouzwa
katika soko la Afrika, kufungua biashara ya bidhaa kwa asilimia 97 na
uanzishwaji wa Sekretarieti ya kusimamia utekelezaji wa Mkataba wa
AfCFTA.
Aidha,
alimpongeza Mheshimiwa Mahamadou Issoufou, Rais wa Jamhuri ya Niger kwa
jitihada zake za kuhakikisha azma ya Umoja wa Afrika ya kuanzisha Soko
Huru la pamoja la Afrika inafikiwa.
Makamu wa Rais pia alizipongeza nchi 27 wanachama wa Umoja huo zilizoridhia mkataba wa uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) kati ya nchi 54 zilizotia saini mkataba huo na kuahidi kwamba Tanzania itaungana nao baada ya kukamilisha taratibu za ndani.
Makamu wa Rais pia alizipongeza nchi 27 wanachama wa Umoja huo zilizoridhia mkataba wa uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) kati ya nchi 54 zilizotia saini mkataba huo na kuahidi kwamba Tanzania itaungana nao baada ya kukamilisha taratibu za ndani.
Kwenye
mkutano huo Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambapo alitoa salam za Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
Wakuu wa Nchi na Serikali waliohudhuria mkutano huo.
Wakati
huo huo Waziri wa Fedha na Uchumi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Mhe. Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa amesema kwa upande wa Afrika
Mashariki Tanzania imepiga hatua zaidi kutokana na kuwepo katika
Jumuiya za Afrika Mashariki na SADC, hivyo Tanzania imefaidika sana
kutokana na kupanuka kwa Soko hilo.
Nae
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiao wa Afrika Mashariki Dkt.
Damas Ndumbaro amesema Tanzania imenufaika na mkutano huo kutokana na
kuendelea kujifunza zaidi kuhusiana na Biashara ya pamoja katika Afrika
pamoja na kuweza kushiriki kuchagua Muwakilishi wa Bara la Afrika katika
nafasi mbalimbali ndani ya Afrika na Duniani kote wakati Tanzania
imepata nafasi moja ambapo Bethabina Seja Afisa wa Takukuru amechaguliwa
katika Bodi ya kudhibiti Rushwa Barani Afrika.
No comments:
Post a Comment