Rais wa Marekani Donald Trump ametoa onyo kali kwa kiongozi wa Korea
Kaskazini Kim Jong un katika hotuba ndani ya bunge la Korea Kusini.
''Usitudharau,
Usitujaribu," alisema, huku akishutumu hali ilivyo nchini Korea Kaskazini.
Bwana Trump
alimzungumzia moja kwa moja rais Kim akisema kuwa ''silaha
unazojilimbikia
hazikufanyi wewe kuwa salama lakini zinakuweka katika hali hatari''.
Kiongozi huyo wa
Marekani yuko katika ziara ya siku mbili nchini Korea Kusini katika ziara ya
bara Asia.
Kwengineko katika hotuba
yake amesema kuwa huku Korea Kaskazini ikiona uvumilivu kuwa udhaifu sasa kuna
utawala mpya nchini Marekani.
Bwana Trump pia ameutaka
ulimwengu hususan China na Urusi kuiwekea shinikizo kali Pyongyang kusitisha
utengenezaji wake wa silaha za kinyuklia.
Dunia haiwezi kuvumilia
hatari inayosababishwa na taifa linaloongozwa na utawala usioaminika ambao
unaitishia na silaha za kinyuklia.
Mataifa yote
yaliowajibika yanafaa kuungana kuangamiza utawala wa kikatili wa Korea
Kaskazini kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeuunga mkono, kupata usaidizi wowote
ama hata kukubalika, alisema.
No comments:
Post a Comment