Rais John Magufuli amemwandikia
barua waziri mkuu wa Canada kuulizia kuhusu ndege ya Bombadier, inayoshikiliwa
nchini humo na kumtaka ashughulike suala hilo kwa haraka.
Akizungumza katika uzinduzi wa
Uwanja wa ndege mjini Bukoba leo Jumatatu
Novemba 6, Rais Magufuli amesema
amemtuma pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju kwenda Canada
kushughulikia suala hilo kisheria.
"Nimemwandikia barua waziri
wa Canada kuulizia kwanini ndege yetu inakaa zaidi ya miezi sita, tumechoka
kusubiri. Nimemtuma pia mwanasheria mkuu ili akapambane nao kisheria,"
amesema.
Amesisitiza kwamba kama wameamua
kupambana kisheria watapambana na amewataka wanasheria wa Tanzania kushikamana
ili kuhakikisha kwamba ndege hiyo inakuja Tanzania.
Rais Magufuli amewaonya wananchi
pia kuacha kuzungumza kwenye mitandao ya kijamii. Alisema “ninawaomba watu wa
vyama vyote waunge mkono juhudi hizi zinazofanywa na serikali.”
Magufuli ambaye ametimiza miaka
miwili tangu achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania amesema ndege zote sita zilizonunuliwa
na Serikali zitakuja.
No comments:
Post a Comment