Picha za wavulana
wawili wa Kichina ambao walisafiri na basi moja kwa umbali wa kilomita
80 wakiwa chini ya gari hilo zilizua hisia kali kuhusu hali ya watoto wa
taifa hilo waliowachwa nyuma.
Wawili hao ambao hawajatajwa na
serikali wanatoka katika kijiji kimoja maskini Kusini mwa Guangxi na
walikuwa wakijaribu kwenda kwa wazazi wao wanaofanya kazi katika mkoa
jirani wa Guangdong.
Waliripotiwa kwamba wametoweka mnamo tarehe
23 Novemba na mwalimu wao na kupatikana siku hiyohiyo chini ya gari hilo
katika kituo kimoja cha mabasi.
Picha na kanda za video zinaonyesha vijana hao waliojaa matope na wakining'inia chini ya basi hilo.
Kulingana
na gazeti la Southern Morning (Nanguo Zaobao), wavulana hao wana umri
wa kati ya miaka minane na tisa na walipatikana na maafisa wa usalama
wakati basi hilo liliposimama katika kituo kimoja.
Walikuwa tayari wamesafiri katika maeneo yenye milima kwa takriban maili tatu huku wafanyikazi hao wakibaini kwamba hawakuumia.
Miili
ya watoto hao ilikuwa myembamba mno hivyobasi eneo la chini la basi
hilo lilikuwa eneo zuri la kujificha , mfanyikazi mmoja aliliambia
gazeti hilo.
Wafanyikazi wanasema kuwa wavulana hao walikataa kuzungumza walipohojiwa.
Lakini
mfanyikazi mmoja aliliambia gazeti la Southern Morning: Baadaye
tulielewa kwamba wavulana hao walikuwa wakitaka kuonana na wazazi wao.
Walijificha chini ya basi hilo kwa sababu walitaka kuwaona wazazi wao.
Ripoti zinasema kuwa watu wa jamii yao waliarifiwa na vijana hao wakachukuliwa siku hiyohiyo.
No comments:
Post a Comment