Korea
Kaskazini imelifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu
lililoruka juu zaidi na kudumu angani kwa dakika 53 kabla ya kutua
katika bahari ya Japani.
Kwa mujibu wa waziri wa maswala ya ulinzi nchini Marekani James Mattis, kombora hilo ni hatari zaidi kwa sababu liweza kutua katika kona yoyote ile ya dunia ikiwemo Marekani.
Komora hilo liliruka kwa urefu wa kilomita 4,500 na kusafiri umbali wa kilomita 960 kulingana na jeshi la Korea Kusini.
Mara
ya mwisho kwa taifa hilo kulifanyia jaribio kombora lake ni mwezi
Septemba. Wakati huo, kombora lake la mwisho lilikuwa la sita la nguvu
za kinyuklia mwezi huo.
Korea Kaskazini imeendeleza mpango wake wa kinyuklia pamoja na ule wa utengenezaji wa makombora licha ya vikwazo ilivyowekewa.
Baraza
kuu la usalama la umoja wa mataifa linatarajiwa kukutana katika kikao
cha dharura ili kuzungumzia hatua hiyo ya kombora lililorushwa jana.
Rais
wa Marekani Donald Trump aliarifiwa kuhusu hatua hiyo wakati ambapo
kombora hilo bado lilikuwa angani ambapo aliishia tu kusema
''Tutalishughulikia''.
No comments:
Post a Comment