Thursday, November 30, 2017

TIMU YA ARSENAL YACHARUKA YAMPIGA MTU MKONO


Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, amempongeza mpambanaji Mesut Ozil baada ya raia huyo wa Ujerumani kuchangia ushindi mnono wa klabu hiyo wa magoli 5-0 dhidi ya Huddersfield.

Ozil alifunga goli moja na kusaidia mengine mawili na kuifanya Arsenal kushinda michezo saba ya Ligi Kuu ya Ungereza katika msimu huu.
           Mshambuliaji Mfaransa Alexandre Lacazette akiifungia Arsenal goli la kwanza
Mohamed Salah ametokea benchi na kufunga mara mbili na kuisaidia Liverpool kupata ushindi wa ugenini wa magoli 3-0 dhidi ya Stoke City na kukwea hadi katika nafsi ya nne.

Winga raia wa Senegal Sadio Mane aliwapatia Liverpool goli la kwanza la utata akitumbukiza mpira wavuni sekunde chache kabla ya refa msaidizi kutoa uamuzi.

Katika mchezo huo Stoke waliamini kipa wa Liverpool, Simon Mignolet, alipaswa kutolewa nje kwa kumchezea rafu mshambuliaji Mame Biram Diouf nje ya boksi.

No comments:

Post a Comment