Thursday, November 30, 2017

KOCHA PEP GUARDIOLA AMWAGIA SIFA RAHEEM STERLING

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, amesema kujiamini kwa Raheem Sterling kumemfanya awe na kiwango bora baada ya kufunga goli la ushindi dhidi ya Southampton katika dakika ya 96.

Goli hilo la Sterling ni la 13 katika msimu huu na limeipa klabu yake ushindi wa 12 katika msimu huu wa Ligi Kuu na kuongoza kwa tofauti ya pointi nane, baada ya mchezo huo kuisha kwa magoli 2-1.
   Mchezaji Oriol Romeu akishangilia baada ya kufunga goli na kufanya matokeo kuwa 1-1
    Raheem Sterling akiifungia Manchester City goli la pili na la ushindi katika dakika za ziada

Kocha wa Chelsea Antonio Conte amemuomba radhi refa Neil Swarbrick baada ya kutolewa nje kwa kupinga maamuzi ya refa katika mchezo ambao Chelsea ilipata ushindi kiduchu wa goli moja.

Kocha huyo raia wa Italia alijikuta katika kipindi chote cha pili akiangalia mchezo huo katika dimba la Stamford Bridge kwa kutumia runinga akiwa katika chumba cha kubadilishia nguo.

No comments:

Post a Comment