Monday, November 13, 2017

Somaliland yapiga kura katika uchaguzi wa urais

Raia wa Somaliland wakipiga kura


Image captionRaia wa Somaliland wakipiga kura

Shughuli ya kupiga kura imeanza katika Jamhuri iliojitangaza ya Somaliland katika uchaguzi wa urais.
Uchaguzi huo utatumia mfumo wa kiteknolijia wa kutambua macho ya kila mpiga kura ikiwa ni mara ya kwanza duniani kulingana na msemaji wa uchaguzi.

Mwanamke aliyeshiriki katika shughuli ya upigaji kura Somaliland
Image captionMwanamke aliyeshiriki katika shughuli ya upigaji kura Somaliland

Zaidi ya wapiga kura 700,000 watapiga kura katika uchaguzi ulio na wagombea watatu.
Takriban wachunguzi 60 wapo nchini humo kuangalia uchaguzi huo.

Baadhi ya wapiga kura wakipanga foleni katika uchaguzi huo
Image captionBaadhi ya wapiga kura wakipanga foleni katika uchaguzi huo

Mmoja ya wachunguzi Susan Mwape kutoka Zambia aliambia BBC kwamba watachunguza kila kitu katika uchaguzi huo ikiwemo utendaji kazi wa maafisa wa shirika linalosimamia uchaguzi huo.
Rashid Abdi kutoka shirila la kitaifa la Crisis aliambia BBC kwamba iwapo Somalia itafanikiwa kufanya uchaguzi huo kuwa huru na wazi basi itaimarisha uwezo wake wa kutaka kuwa taifa huru.

Baadhi ya wana habari nao wakijiandaa kuchukua habari za shughuli hiyo ya upigaji kura Somaliland
Image captionBaadhi ya wana habari nao wakijiandaa kuchukua habari za shughuli hiyo ya upigaji kura Somaliland

Ameitetea serikali kwa kuzima mitandao ya kijamii ili kuzuia kusambaa kwa habari bandia na zile zisizosahihi wakati wa kipindi chote cha uchaguzi.
Somaliland ilijitangaza kuwa huru baada ya kupinduliwa kwa aliyekuwa rais wa Somalia Siad Barre 1991.

Maafisa wa usalama wakihakikisha kuwa kuna amani wakati wa shughuli hiyo ya kihistoria
Image captionMaafisa wa usalama wakihakikisha kuwa kuna amani wakati wa shughuli hiyo ya kihistoria

No comments:

Post a Comment