Wanachama
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza, wanakusudia kufanya
maandamano ya amani Aprili 26, mwaka huu, kuunga mkono na kupongeza kazi
kubwa inayofanywa na Rais Dkt John Pombe Magufuli
Maandamano
hayo yanakuja ikiwa ni jitihada za kuzima kile walichokiita uhuni
unaofanywa na wapinzani wao kisiasa wa kutaka kuharibu amani kwa
kuhamasisha maandamano ya kuchochea vurugu siku hiyo kupitia mitandao ya
kijamii.
Kauli
hiyo ilitolewa juzi na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Mwanza, Paschal
Mwangwala wakati wa kikao maalumu cha uwasilishaji wa taarifa ya
utekelezaji wa kazi za Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Angelina Mabula kwa
miaka miwili uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kiruma, jijini Mwanza na
kuhudhuriwa na wajumbe 608 kati ya 748 kutoka kata 19 za jimbo hilo.
Mangwala
alisema wana-CCM hawawezi kukaa kimya na kushangilia vitendo
vinavyofanywa na wapinzani vya kutaka kuvunja amani, bali wazuie kwa
kuandaa maandamano hayo yatakayoeleza kuwa chama pekee nchini ni CCM.
“Saidieni
watu waone chama ni CCM peke yake na si vingine vinavyodandia ajenda ya
kupiga kelele hiyo Aprili 26, na sisi tusaidiane maandamano ya
kumpongeza Rais Magufuli. Haiwezekani watu waongee vitu vya kipuuzi na
kukaa kimya.”
“CCM
Mwanza hatuwezi kuvumilia yeyote atakayevunja amani, yeyote atakayeleta
chokochoko kwenye mkoa wetu atakiona cha mtema kuni. Yanayofanywa na
viongozi wetu wa juu yashuke mpaka kule chini, wananchi waone, viongozi
wa mitaa waunge juhudi hizi,” alisema.
Mwenyekiti
wa CCM wilaya ya Ilemela, Nelson Mesha alisema kinachofanywa na vyama
vya upinzani nchini ni dalili tosha kuwa vimefikia mwisho na vimekosa
hoja na badala yake vinakimbilia kufanya maandamano.
No comments:
Post a Comment