Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum Jijini Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, ametolea
ufafanuzi suala ambalo limeanza kushika hatamu mitandaoni la kukamatwa
kwa Katibu wa Baraza la Wanawake CHADEMA kata ya Kisutu Elizabeth
Mambosho na kupelekwa rumande akiwa na mtoto mchanga.
Kamanda
Mambosasa amesema mwanamke huyo alishaachiwa kwa dhamana, na kwamba
kesi yake inachunguzwa na makao makuu, licha ya kutoweka wazi sababu ya
kukamatwa kwake.
“Alikamatwa
wakati mimi nipo safarini na alishadhaminiwa, na kesi yake inapelelezwa
makao makuu, lakini sijui sababu ya kukamatwa kwake labda muwaulize
makao makuu”, amesema Kamanda Mambosasa.
Taarifa
za kukamatwa kwa Elizabeth zimezagaa mitandaoni huku watu wakilalamikia
kitendo cha kukamatwa akiwa na mtoto wake mchanga aliyejifungua wiki
tatu zilizopita, huku akiwa na mshono kwani imeelezwa alijifungua kwa
njia ya upasuaji.
by richard shiyo/rich voice
No comments:
Post a Comment