Ubalozi
wa Marekani nchini umetoa tahadhari kwa wananchi wao wanaoishi Tanzania
kuhusu maandamano ya kisiasa yanayotarajiwa kufanyika Aprili 26.
Maandamano
hayo yanatarajiwa kufanyika siku ya Muungano huku baadhi ya wanasiasa
wakiwa tayari wameshafunguliwa kesi mahakamani kutokana na tuhuma
mbalimbali.
Ubalozi
umetoa tahadhari kwa raia wake wote kwamba siku ya Aprili 26 wanatakiwa
kuwa makini kwa sababu inawezekana kabisa maandamano yakatokea.
Kwenye taarifa hiyo ambayo imetolewa kwa vyombo vya habari imesema kwamba polisi wamejiandaa kukabiliana na maandamano hayo.
“Polisi
wanaweza wakatumia mabomu ya machozi na risasi za moto ili kudhibiti
maandamano hayo hivyo ni muhimu kukaa mbali na waandamanaji hao.
Serikali
ya Marekani inawatakia kila la kheri raia wa Marekani kwa kuwataka
kukaa mbali na makundi ya watu siku hiyo ya Aprili 26 na kufuatilia
taarifa kwenye vyombo vya habari ili kujua kinachoendelea.
by richard shiyo/rich voice
No comments:
Post a Comment