Serikali ya Syria na mshirika wake Urusi zimeishutumu Israel kwa shambulio baya katika uwanja wa ndege za kijeshi za Syria.
Shambulio
hilo la Jumatatu liliulenga uwanja wa ndege za kivita wa Tiyas
unaofahamika kwa umaarufu kama T4, karibu na mji wa Homs. Waangalizi
wanasema watu 14 wameuawa.
Israel, ambayo awali iliwahi kuyelnga
maeneo nchini Syria bado haijatoa tamko lolote. Awali Syria iliilaumu
Marekani kwa shambulio hilo.
Tukio hilo limetekelezwa huku jamii
ya kimataifa ikiendelea kulaani shambulio la kemikali ambalo
lilitekelezwa katika mji wa Douma ambao unashikiliwa na waasi. Marekani
na Ufaransa zimetishia kulipiza kisasi.
Rais wa Marekani Donald
Trump alimweleza Rais wa Syria kama "nduli" Jumapili na kuonya kwamba
yeye pamoja na washirika wake Iran na Urusi "watalipia sana".
Bw Trump na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron walitoa taarifa siku
hiyo na kuapa "kuchukua hatua kali na ya pamoja" kuhusiana na shambulio
hilo.
Lakini maafisa wa Marekani wamekanusha uwezekano kwamba Marekani ndiyo iliyotekeleza shambulio hilo.
"Kwa sasa, Wizara ya Ulinzi haitekelezi mashambulio yoyote ya angani Syria," Pentagon imesema kupitia taarifa.
"Hata
hivyo, tunaendelea kufuatilia kwa karibu na kuunga mkono juhudi za
kidiplomasia zinazoendelea za kuwawajibisha wote wanaotumia silaha za
kemikali, nchini Syria na kwingineko, kuhakikisha wanaadhibiwa."
Aprili mwaka 2017, Marekani ilirusha makombora 59 aina ya Tomahawk
katika uwanja wa ndege za kivita wa Shayrat nchini Syria baada ya
shambulio la kemikali kutekelezwa katika mji wa Khan Sheikhoun uliokuwa
unashikiliwa na waasi.
Israel ilitekeleza pia mashambulio mengine makubwa dhidi ya Syria mapema mwezi huu.
Nini kilitokea Douma?
Duru za kimatibabu zinasema watu wengi walifariki katika shambulio hilo la Douma, mlinalopatikana Ghouta Mashariki.
Video
moja ambayo imekuwa ikisambaa ambayo ilirekodiwa na wahudumu wa
kujitolea wafahamikao kama White Helmets linawaonesha maiti za wanaume,
wanawake na watoto kadha ndani ya jumba moja, maiti nyingi zikiwa na
povu mdomoni.
Hata hivyo, imekuwa vigumu kubaini hasa nini kilitokea na idadi kamili ya waliofariki.
Syria na Urusi wote wamekana taarifa kwamba shambulio la kemikali
lilitekelezwa, na wameafikiana mkataba wa kuwahamisha waasi ambao
walikuwa wakishikilia mji wa Douma.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kukutana Jumatatu kujadili mzozo huo.
No comments:
Post a Comment