Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewataka wananchi wote
kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwa kuwa maandamano
yanayozungumzwa hayapo na ni batili.
Akizungumza
leo Jumatano Aprili 25 na shirikisho la waendesha bodaboda Mkoa wa Dar
es Salaam, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, ACP Sweethbert Njwele
amesema jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha kila mtu anafanya
shughuli zake kama kawaida bila uvunjifu wowote wa amani.
"Niwahakikishie
jeshi la polisi tumejipanga na mkoa wetu utaendelea kubaki salama
hakuna maandamano yatakayofanyika hivyo kila mtu aendelee na shughuli
zake kama kawaida," amesema Njwele.
Amesema
waendesha bodaboda ni kundi kubwa ila kuna baadhi yao si waaminifu na
kutaka wajiepushe na watu watakaowashawishi kuvunja sheria za nchi.
Kwa
upande wake, Msemaji wa Shirikisho hilo Adamu Kyando amesema uvumi
unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Aprili 26 bodaboda
watashiriki si kweli kwani hakuna bodaboda yeyote atakayeshiriki
maandamano hayo.
"Kuna
taarifa zinazosambaa kwenye mitandao yakijamii ikihamasisha bodaboda
kushiriki maandamano taarifa hizi si za kweli na ni batili," amesema
Kyando.
Amesema
kwa yeyote atakayeshiriki maandamano hayo uongozi hautahusika kwani
taarifa zinazosambazwa hazitoki kwenye shirikisho hilo.
by richard shiyo/rich voice
No comments:
Post a Comment