Rais
Donald Trump amesema Marekani inapanga kutoa jibu la nguvu kuhusiana na
shambulio la kemikali katika mji wa Douma nchini Syria.
Rais Trump ambaye amekutana na washauri wake wa kijeshi amesema uamuzi unaweza kuchukuliwa katika saa zijazo.
Kauli yake hiyo inafuatia kauli mbalimbali za kulaani shambulio hilo ziliotolewa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Wakati wa kikao hicho, Urusi na Marekani zilijikuta zikitupiana vikali maneno.
Balozi
wa Marekani katika baraza hio Nikki Haley amemtuhumu Rais wa Syria
Bashar al Assad kwa jinsi alivyowajibika kwa shambulio hilo.
Ametaka
kupigwa kura hii leo, juu ya azimio la awali kuweza kufanya uchunguzi
mpya juu ya matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria.
Tayari Urusi ambaye ndiye mshirika wa Syria imesema haita unga mkono pendekezo hilo.
Mwakilishi
wa Urusi, Vassily Nebenzia amesema tukio lililotokea katika mji wa
Douma ni la kupangwa, na kwamba hatua za kijeshi zinazotaka kuchukuliwa
na Marekani zinaweza kuwa na athari mbaya.
Akitoa
kauli ya nchi yake, Rais Trump amesema tukio hilo litakutana uamuzi
aliouita wa nguvu na kuongeza kuwa nchi yake ina njia na maamuzi mengi
ya kijeshi na kwamba hatua zitachukulkiwa katika kipindi kifupi.
Naye
Mwakilishi wa Syria katika Umoja wa Mataifa Bashar Jaafari amesema
Marekani na washirika wake wamekuwa wakifadhili ugaidi nchini Syria, na
ndio wao wanapaswa kuwajibika na shambulio hilo la kemikali.
Kufuatia
kikao hicho cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kauli
iliyotolewa na Rais Donald Trump, kumekuwa na dalili zinazoonesha kuwa
mataifa ya magharibi yataungana na Marekani kupanga hatua za kuchukua.
No comments:
Post a Comment