Mkurugenzi
mtendaji wa taasisi hiyo, Dk Donald Mmari alisema jana kuwa, pamoja na
Serikali kushughulikia ukuaji wa uchumi kwa miaka 15 iliyopita, tafiti
mbalimbali zinaonyesha viwango vya tija katika sekta nyingi ziko chini.
“Lakini
pia hata ushindani wake ukilinganisha na nchi nyingine bado
hauridhishi, Tanzania inao uwezo wa kujiweka katika nafasi kubwa zaidi
kiuchumi duniani kutokana na upatikanaji wake katika jiografia, wingi wa
rasilimali za asili, utulivu wa kisiasa na kijamii,”alisema.
Baadhi
ya vikwazo alivyotaja katika mkutano wa waandishi wa habari ni pamoja
na upatikanaji wa nguvu kazi yenye afya, ujuzi na elimu, miundombinu
rafiki ya biashara na uwekezaji.
Wachumi
kutoka taasisi mbalimbali, NGO, viongozi, wasomi, wahisani na watunga
sera wametajwa kushiriki warsha itakayofanyika leo na kesho
itakayojikita katika uzalishaji wenye tija na ushindani katika
utandawazi.
Warsha
hiyo itaongozwa na katibu mtendaji wa Shirikisho la Forodha la Kusini
mwa Afrika (Sacu), Pauline Mbala huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.).
Masuala
yatakayojadiliwa yatajikita kwenye mabadiliko ya mfumo wa uchumi
hususan katika umuhimu wa kufahamu misingi ya uzalishaji wenye tija na
ushindani katika utandawazi na masoko
Mtafiti
mwandamizi katika taasisi hiyo, Dk Blandina Mlama alisema ni umuhimu
pia kuwekeza katika mnyororo wa thamani kupitia sekta zinazoajiri
Watanzania wengi.
No comments:
Post a Comment