Tanzania
inakadiriwa kuwa na wafungwa 40,000 wakati uwezo wa magereza yake ni
30,000 hivyo kuna ongezeko la zaidi ya wafungwa 10,000 katika msongamano
huo.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri Hamad Yusufu Masauni wakati akijibu
swali la nyongeza la Ruth Mollel ambaye ametaka kujua Serikali inafanya
nini kumaliza msongamano wa wafungwa.
Masauni amesema kuna ongezeko la zaidi ya wafungwa 10,000 ambapo kwa sasa Serikali inafanya kila namna kumaliza msongamano huo.
Katika
swali la msingi Mwantakaje Haji Juma (BUBUBU-CCM) amehoji ni lini
kituo cha polisi katika jimbo lake kitafanyiwa ukarabati.
Naibu Waziri amesema kituo hicho kitafanyiwa kazi wakati wowote fedha ikipatikana ili kiwawezeshe askari kutoa huduma bora.
No comments:
Post a Comment