Manchester City wako tayari kumuuza mlinzi wa England John
Stones, mwenye umri wa miaka 23, msimu huu wa joto. (Sun)
Mshambuliaji
wa Tottenham Fernando Llorente, mwenye umri wa miaka 33, ana nafasi ya
kuondoka katika klabu hiyo na huedna akajiunga tena na klabu yake ya
zamani Athletic Bilbao. (Mirror)
Manchester City wanaongoza
jitihada za kumsajili mchezaji wa Napoli raia wa Italia mwenye umri wa
miaka 26 Jorginho na mabingwa hao wa Premier League wamefanya mazungumzo
ya kina na wawakilishi wa mchezaji huyo. (Mail)
Mrithi wa Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal
itabidi atumei bajeti ndogo msimu huu wa joto ya kiasi ya £ milioni 50.
(Telegraph)
Mkurugenzi mtendaji wa Arsenal Ivan Gazidis anaamini
kuwa kapteni wa zamani wa Gunners Mikel Arteta, mwenye umri wa miaka 36,
ambaye sasa ni kocha katika timu ya Manchester City, huenda akawa
ndiye mrithi wa Arsene Wenger. (Sky Sports)
Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Arsenal Ray Parlour
anaamini kuwa Meneja wa Newcastle Rafael Benitez huenda ndiye
anayestahili kumrithi Arsene Wenger. (Talksport)
Arsene Wenger
huenda atakuwa na nia ya kuisimamia timu ya taifa ya England siku moja
anasema mwandishi wa soka ya Ufaransa Julien Laurens. (BBC Radio 5 live)
Burnley wana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa West Brom Jay Rodriguez, mwenye umri wa miaka 28, arudi Turf Moor. (Mail)
Leicester
City inafikiria kumsajili beki wa kulia wa timu ya Porto raia wa Ureno
Ricardo Pereira, mwenye umri wa miaka 24. (Leicester Mercury)
Meneja
wa Stoke Paul Lambert na mkurugeniz anayehusika na usajili Mark
Cartwright wanatarajiwa kusalia msimu ujao hata kama timu hiyo
itashushwa daraja. (Stoke Sentinel)
Rais wa Roma James Pallotta
anasema klabu hiyo haitaki kumuuza kipa raia wa Brazil Alisson, mwenye
umri wa miaka 25, ambaye amekuwa akilenga na Liverpool. (Sky Sport
Italia )
Majadiliano kuhusu kuiuza klabu ya Newcastle United
kwenda kwa Amanda Staveley yatapiga hatua katika mwezi ujao iwapo
wanatafuta nafasi ya kupata ufanisi. (Sky Sports)
Adam Pearson, mmiliki wa klabu ya Hull FC ya raga anaongoza mchakato wa kuinunua Sunderland. (Sun)
Kapteni wa West Brom Chris Brunt, mwenye umri wa
miaka 33, amesaini mustakabali wake kwa klabu hiyo na mchezaji huyo wa
kiungo cha kati anatarajia wachezaji wengine wakuu watafuata mfano wake
licha ya uwezekano wa timu hiyo kushushwa daraja katika
ubingwa.(Birmingham Mail)
Huenda Liverpool ikahifadhi mamilioni ya
pauni kwa mchezaji Naby Keita, mwenye umri wa miaka 23, wakati mchezaji
huyo raia wa Guinea atakapojiunga na timu hiyo katika msimu ujao wa
joto - ikiwa ni kutokana na matokeo duni ya RBLeipzig msimu huu.
(Liverpool Echo)
Swansea wamejiunga na Celtic na Rangers katika
kumsaka mchezaji wa Dundee raia wa Finland mwenye umri wa miaka 22 Glen
Kamara. (Sun)
chanzo-bbc swahili
by richard shiyo/rich voice
No comments:
Post a Comment