Marekani imeyataka
mataifa yote kukatiza uhusiano wa kidiplomasia na ule wa kibiashara na
Korea Kaskazini baada ya taifa hilo kufanyia jaribio la kombora lake la
masafa marefu.
Thursday, November 30, 2017
KOCHA PEP GUARDIOLA AMWAGIA SIFA RAHEEM STERLING
TIMU YA ARSENAL YACHARUKA YAMPIGA MTU MKONO
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger,
amempongeza mpambanaji Mesut Ozil baada ya raia huyo wa Ujerumani
kuchangia ushindi mnono wa klabu hiyo wa magoli 5-0 dhidi ya
Huddersfield.
Wednesday, November 29, 2017
Korea Kaskazi Yarusha Kombora La Masafa Marefu Zaidi Linaloweza Kutua Sehemu Yoyote Duniani
Korea
Kaskazini imelifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu
lililoruka juu zaidi na kudumu angani kwa dakika 53 kabla ya kutua
katika bahari ya Japani.
TANESCO Wataja Chanzo cha Kukatika kwa Umeme Dar, Pwani
Shirika
la Umeme Tanzania (Tanesco) limetoa taarifa kwa wateja katika mikoa ya
Dar es Salaam na Pwani kuwa baadhi ya maeneo hayana umeme kutokana na
hitilafu iliyojitokeza.
Tundu Lissu Asimulia Alivyonusurika Kupigwa Risasi ya Fuvu la Kichwa
Kwa
mara ya kwanza, Tundu Lissu amezungumzia shambulio la kinyama
alilofanyiwa na watu wasiojulikana kwa kueleza kuwa, alinusurika
kufumuliwa fuvu la kichwa kwa risasi.
Tuesday, November 28, 2017
Wavulana 2 wasafiri kilomita 80 chini ya basi China
Picha za wavulana
wawili wa Kichina ambao walisafiri na basi moja kwa umbali wa kilomita
80 wakiwa chini ya gari hilo zilizua hisia kali kuhusu hali ya watoto wa
taifa hilo waliowachwa nyuma.
Mabasi ya Mwendokasi Dar Yageuka shule kwa nchi za Afrika.....Dart Yapanga kuongeza mabasi Mengine 165
Tangu
kuanza rasmi Mei 10, 2016 kwa mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini
Dar es Salaam, zaidi ya nchi tano za Afrika zimetuma viongozi wake
kujifunza namna ya uendeshaji wake.
IGP Sirro Atembelea Bandarini Kufanya Ukaguzi wa Magari ya Polisi Yaliyoibuliwa na Rais Magufuli
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amefanya ziara katika
bandari ya Dar es salaam, ili kufanya ukaguzi wa magari 31 ya Jeshi hilo
ambayo Mhe. John Pombe Magufuli, alielekeza kukabidhiwa kwa Jeshi hilo
ili kurahisisha utendaji kazi
Tuesday, November 21, 2017
Monday, November 20, 2017
Mugabe akataa kuachia madaraka Zimbabwe licha ya shinikizo
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameapa kuendelea kuongoza taifa hilo kwa wiki kadha, licha ya shinikizo kutolewa kumtaka aachie madaraka.
Akihutubu moja kwa moja kupitia runinga ya taifa, Bw Mugabe amesema anapanga kuongoza mkutano mkuu wa chama mwezi Desemba.
Maafisa wakuu wa chama hicho cha Zanu-PF walikuwa wameidhinisha hatua ya kumvua uongozi wa chama hicho na kumpatia saa 24 ajiuzulu la sivyo wamuondoe madarakani.
Jeshi lilichukua udhibiti wa serikali wiki iliyopita, huku mzozo kuhusu nani atamrithi ukizidi kutokota. Bw Mugabe ameonekana kupoteza udhibiti wa chama chake.
Mzozo wa sasa ulianza Bw Mugabe alipomfuta kazi makamu wake Emmerson Mnangagwa wiki mbili zilizopita, hatua iliyolikera jeshi ambalo lilitazama hatua hiyo kama jaribio la kumteua mke wake Grace kuwa makamu wa rais na mwisho kuwa mrithi wake.
Amekiri uokosoaji dhidi yake kutoka kwa Zanu-PF, jeshi na umma, na kusisitiza kwamba ipo haja ya hali ya kawaida kurejea.
"Bila kujali faida au madhara ya jinsi (jeshi) walitekeleza operesheni yao, mimi, kama amiri jeshi mkuu, nakiri kwamba kuna matatizo," amesema, akirejelea hatua ya jeshi ya kuchukua udhibiti wa runinga ya taifa wiki iliyopita.
Hata hivyo, hakuzungumzia uwezekano wake kujiuzulu.
Raia wengi nchini Zimbabwe wameonekana kushangazwa na hotuba ya Bw Mugabe ambaye alitarajiwa na baadhi yao kujiuzulu.
Kiongozi wa chama chenye ushawishi cha maveterani wa vita vya ukombozi wa Zimbabwe Chris Mutsvangwa, ameambia shirika la habari la AFP kwamba sasa Robert Mugabe huenda akaondolewa madarakani baada yake kukosa kujiuzulu leo.
Amesema hotuba ya kiongozi huyo haijazingatia uhalisia.
"Tutafuata njia ya kumuondoa madarakani na tunawataka watu warejee tena barabarani kuandamana."
Maveterani walikuwa wakati mmoja wafuasi sufu wa Bw Mugabe.
Waliongoza uvamizi wa mashamba yaliyomilikiwa na Wazungu mwaka 2000 na wametuhumiwa kwa kutumia ghasia na fujo uchaguzini kumsaidia Mugabe kusalia madarakani.
Lakini mwaka jana, waliacha kumuunga mkono.
Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai ambaye wakati mmoja alihudumu kama waziri mkuu katika serikali ya umoja wa taifa na Rais Robert Mugabe ameambia shirika la habari la Reuters kwamba ameshangazwa sana na hotuba ya Mugabe.
Sawa na baadhi ya raia wengine Zimbabwe, kiongoz
Mahakama Kuu Kenya Yatupilia Mbali Kesibza Kupinga Ushindi wa UhurubKenyatta
Mahakama ya Juu nchini Kenya imetupilia mbali kesi zilizofunguliwa na wafuasi wa NASA za kupinga ushindi wa Urais wa Uhuru Kenyatta, kwenye uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26, 2017
Monday, November 13, 2017
Wednesday, November 8, 2017
DONALD TRUMP: USITUDHARAU, USITUJARIBU.
Rais wa Marekani Donald Trump ametoa onyo kali kwa kiongozi wa Korea
Kaskazini Kim Jong un katika hotuba ndani ya bunge la Korea Kusini.
''Usitudharau,
Usitujaribu," alisema, huku akishutumu hali ilivyo nchini Korea Kaskazini.
Bwana Trump
alimzungumzia moja kwa moja rais Kim akisema kuwa ''silaha
NAIBU WAZIRI WA MUNGANO NA MAZINGIRA, AMEWATAKA WANANCHI KUTOITAFSIRI VIBAYA.
Naibu waziri wa Mungano na Mazingira Kangi Lugola, amewataka wananchi kutoitafsiri vibaya kauli ya Rais kuhusu kufanya shughuli za kilimo kwenye vyanzo vya maji, na kusema kwamba hakuna sheria inayoruhusu watu kufanya shughuli za kilimo.
Waziri Lugola ameyasema hayo leo alipokuwa akijibu swali Bungeni kuhusu kauli hiyo ya Rais ambayo imeonekana kuruhusu watu kufanya uharibifu kwenye vyanzo vya maji na mazingira, na kusema kwamba
“Niwahakikishie kauli ya Rais isije ikapotoshwa wananchi wakaenda kuvamia maeneo ya mito na kuanza kulima, na kauli aliyoitoa Mheshimiwa Rais,
Tuesday, November 7, 2017
SERIKALI YATOA HEKTA 271,882.86 KWA AJILI YA SHUGHULI ZA VIJANA.
Serikali kupitia Halmashauri za Wilaya katika mwaka 2016 imetoa jumla ya Hekta 271,882.86 za ardhi kwa vijana nchi nzima ili kufanya shughuli za uzalishaji mali na kujipatia ajira.
Hayo yameelezwa jana, Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu
RAIS MAGUFULI AAMURU WATU WATATU WACHUNGUZWE KWA KUTAKA KUIIBIA SERIKALI MABILIONI
Rais Dk. John Magufuli, ameamuru kukamatwa kwa watumishi watatu wa serikali, kwa tuhuma za kuandika madai yasiyo halali, kwa lengo la kuiibia serikali.
Rais Magufuli ametoa amri hiyo wakati akizindua Uwanja wa Ndege wa Bukoba wenye urefu wa kilomita 1.5 ambapo amewataja watumishi hao kuwa ni Jackson Kaswahili Robert, Mwachano Msingwa na Gidioni Zakayo.
Alifafanua kwamba, Jackson alijaza fomu zinazoonesha kwamba anaidai serikali
Monday, November 6, 2017
RAIS MAGUFULI AZUNGUMZIA NDEGE YA BOMBADIER ILIYOZUIWA CANADA
Rais John Magufuli amemwandikia
barua waziri mkuu wa Canada kuulizia kuhusu ndege ya Bombadier, inayoshikiliwa
nchini humo na kumtaka ashughulike suala hilo kwa haraka.
Akizungumza katika uzinduzi wa
Uwanja wa ndege mjini Bukoba leo Jumatatu
Sunday, November 5, 2017
Subscribe to:
Posts (Atom)