Tuesday, October 10, 2017

IPO SIRI KUBWA NDANI YA UPAKO ANAOTUMIKA NAO MTU:NABII MKUU MH DK. GEORDAVIE.

LOS ANGLES, MAREKANI
Nabii mkuu Mh Dk. GeorDavie Amewataka watu kutambua kwamba ipo siri kubwa ndani ya upako anaotumika nao mtu, huku akieleza kuwa siri hiyo ni kati ya mwenye upako na Mungu pekee.
Nabii mkuu ameyase hayo wakati akifundisha katika ibada ya Jumapili katika
tawi la Ngurumo Ya Upako Marekani Lililopo Los Angeles nchini humo.
Aidha Mh Dr GeorDavie, amebainisha kuwa Mungu humtuma nabii kwa sababu maalumu, na kumpa kusudi atakalolibeba kwa ajili ya kizazi husika, hivyo ni lazima manabii kuheshimika kulingana na wakati husika.
Mbali na hayo amesema kuwa kila kitu halisi kina mfano wake ambao ni bandia, na ni ukweli kwamba wapo manabii wa uongo, ila pia hakuna haja ya kuwa na mashaka juu ya manabii kwani hata huduma nyingine kati ya huduma tano wapo watumishi wa uongo.

Nabii mkuu Mh Dr GeoDavie yupo nchini marekani kwa Ziara ya mwezi mmoja ambapo wiki ya kwanza aliongoza Kongamano la Upanyaji Kinabii kwa siku mbili, jana ameongoza ibada ya jumapili na anatarajiwa kuhudumia tena ibada kama hiyo jumapili ijayo ya tarehe 15.

No comments:

Post a Comment