Kocha
Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Sweden, Mariane Sundhage Oktoba
23, 2017 amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk. Kebwe Stephen Kebwe
katika Ofisi ya Mkoa na kufanya mazungumzo yenye lengo la kuboresha soka
la wanawake nchini.
Kadhalika,
Kocha Mariane Sundhage amefanya mazungumzo yanayofanana na Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Wallace Karia ambaye baadaye
aliongozana naye kwenda kuangalia Kliniki kwenye Chuo cha Maendeleo ya
Wananchi Bigwa.
Katika
Kliniki hiyo, mbali ya Rais Karia wengine waliokuwako kushuhudia
kliniki hiyo ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka la Wanawake (TWFA), Amina
Karuma na Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya soka la Wanawake, Mia
Mjengwa.
Kocha
Mariane Sundhage yuko nchini Tanzania na kesho Jumanne Oktoba 24, 2017
anatarajiwa kuwa na kliniki maalumu kwenye Uwanja wa Karume, Ilala
jijini Dar es Salaam.
Kocha huyo mahiri ambaye mbali ya Sweden ambako anafundisha sasa, tayari alikwisha kuzinoa timu za taifa za Marekani na China.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Salum Madadi, kliniki hiyo itaanza saa 3.30 asubuhi mpaka saa
6.00 mchana baada ya hapo kocha huyo atakuwa na nafasi ya kuzungumza na
wanahabari.
“Karibu
sana wanahabari kesho kushuhudia ufundi wa Kocha Pia Sundhage akizinoa
baadhi ya timu ambazo TFF imezialika wakiwamo wachezaji wa timu ya
taifa,” amesema Madadi alipokuwa anatambulisha ziara ya kocha huyo.
No comments:
Post a Comment