Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda jana Oktoba 22
amekabidhi Magari ya kisasa 18 kati ya 26 yaliyopelekwa Mkoani
Kilimanjaro yakiwa Mabovu (Mkweche) kwaajili ya kufufuliwa upya.
Magari hayo yalipelekwa Kilimanjaro yakiwa yamebebwa kutokana na ubovu lakini sasa yanarejea Dar es Salaam
yakiwa Mazima na Mwonekano kama Magari ya UN ambapo yatakuwa na uwezo wa kubeba Askari 11 wakiwa wamekaa na silaha zao.
Akikabidhi
Magari hayo kwa Jeshi la Polisi leo RC Makonda amesema yataenda
kuhudumia Wananchi kwa kuimarisha Ulinzi na Usalama jijini Dar es
Salaam.
Amesema
kuwa kilichomgusa kuboresha Jeshi la Polisi ni Baada ya kuona Askari
wakifanya kazi katika mazingira magumu na wakati mwingine kuvamiwa na
majambazi kisha kuuawa na kuporwa Silaha.
Aidha
RC Makonda ameishukuru kampuni ya Rajinder Motors Ltd (RSA) kwa
kumuahidi kutengeneza Magari 56 ya Polisi Dar es Salaam bila kutumia
fedha za serikali (Bure).
Makonda
ametumia Makabidhiano hayo kutuma salamu kwa Majambazi, Vibaka na wale
wenye nia ya kuvuruga Amani na Usalama kuwa kiama chao kimefika.
Amesema alipotangaza mpango wa kufufua Magari yaliyokufa wapo waliombeza lakini sasa wanajionea Magari yakiwa Mapya.
Makabidhiano
hayo yameshuhudiwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira,
Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Dar ea Salaam Lazaro Mambosasa na
viongozi wengine wa vyombo vya Ulinzi na Usalama ambapo wamempongeza RC
Makonda kwa ubunifu mkubwa alionao.
No comments:
Post a Comment