Mkazi wa jijini Dar es Salaam, Robert Massawe (51), ambaye
polisi wanadai ni mtuhumiwa wa uporaji na mauaji, ameuawa kwa kupigwa risasi na
watu wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wenzake.
Kabla ya kuuawa katika majibizano ya risasi, mtuhumiwa
huyo anadaiwa alikamatwa akiwa na SMG yenye risasi 24, simu 19 zilizoporwa
maeneo mbalimbali na laini za simu 58.
Taarifa iliyotolewa jana Jumanne na Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Kilimanjaro,
Hamisi Issah imesema mtuhumiwa aliuawa na wenzake saa tisa usiku wa kuamkia jana wilayani Rombo.
Hamisi Issah imesema mtuhumiwa aliuawa na wenzake saa tisa usiku wa kuamkia jana wilayani Rombo.
Alisema mtuhumiwa pamoja na mkewe walikamatwa jijini Dar
es Salaam na baada ya kuhojiwa na polisi inadaiwa alieleza matukio ya ujambazi
aliyoshiriki na alikubali kuwaonyesha mahali alipoficha bunduki.
Polisi imesema simu tatu kati ya 19 wamegundua ziliporwa
Moshi na moja alikuwa akiitumia mkewe ambaye anashikiliwa Dar es Salaam.
Kamanda Issah alisema aliwaeleza polisi kuhusu mpango wa
kufanya tukio la ujambazi katika Kijiji cha Chilio, Kata ya Holili wilayani
Rombo jana alfajiri.
Alisema askari walifuatana naye chini ya ulinzi hadi Moshi
kwenye dampo lililopo jirani na kiwanda cha ngozi ambako bunduki ilifukiwa
ardhini ikiwa na risasi 24.
“Chini ya ulinzi wa askari kanzu, alipowaona wenzake
alipiga kelele kuwajulisha polisi walikuwepo eneo hilo,” alisema.
Kamanda Issah alisema kelele ziliwafanya watuhumiwa hao
kukimbia huku wakifyatua risasi hovyo na baadhi zilimpiga Massawe mkono wa
kushoto, mgongoni na mguuni hivyo kusababisha kifo chake.
Polisi imesema mtuhumiwa alishiriki matukio manane ya
uporaji wa fedha na mauaji kwa kutumia silaha na amewahi kufungwa kwa ujambazi
lakini aliachiwa baada ya kukata rufaa.
No comments:
Post a Comment