Wednesday, October 4, 2017

NABII MKUU DK. GEORDAVIE KUHUDUMIA MAREKANI JIMAPILI YA TAR 8 MWEZI HUU.



LOS ANGELES, MAREKANI 

Nabii mkuu mh Dr GeorDavie jumapili hii anatarajiwa kuongoza ibada ya kinabii Nchini marekani katika tawi la Ngurumo ya Upako Los Angeles.















Akitoa taarifa kuhusu ibada hiyo msimamizi wa tawi hilo Mtume Katherin,
amesema kuwa watu wa marekani wamepata nafasi ya kuwa na nabii mkuu katika ibada mbili za jumapili, ambapo atakuwa nao jumapili hii ya tarehe 8 na tarehe 15 mwezi huu.

Aidha amesema kuwa wiki hii imekuwa ya Baraka kwao, hasa baada ya kupokea Baraka, mafundisho na kushuhudia Ishara ,Ajabu, Na Miujiza kutoka kwa Nabii mkuu katika kongamano la uponyaji kinabii na wanatarajia mengi  kwa ibada zijazo.

Nabii mkuu Dr GeorDavie, ameondoka nchini Tanzania tarehe 28 mwezi huu kwa ziara ya mwezi mmoja ambapo mwanzoni mwa wiki hii amefanya makongamano mawili katika mji wa Los Angelous na atatembelea maeneo mbalimbali nchini humo ikiwa ni pamoja na kufanya kongamano lingine la kinabii Nchini kanada kabla ya kurejea Tanzania mwezi ujao na kuongoza ibada ya jumapili ya tarehe 5 mwezi wa kumi na moja.



No comments:

Post a Comment