Hayo
yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Katibu wa Kamati hiyo Bw. Wilson
Maage alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, juu ya uzinduzi wa
shindano hilo ambalo litafanyika kwa muda wa miezi miwili.
“Tuzo
hizo zimetokana na kuwepo wazo bunifu (intellectual property) ambalo
azma yake ni kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za huduma na maendeleo
kwa wananchi wa Tanzania na kupima kasi ya utekelezaji wa shughuli hizo
kwa viongozi wa ngazi mbalimbali katika sekta na taasisi za kiserikali
hapa nchini,” alifafanua Maage.
Aliendelea
kusema kuwa, vigezo vitakavyotumiwa katika kuteua viongozi hao ambao ni
wabunge pamoja na Mawaziri ni pamoja na kuwa mtetezi wa Wananchi wake
bila uoga akiwa ndani au nje ya Bunge, mtendaji bora wa maendeleo yenye
kuonekana, sifa ya kutoa hoja zenye tija kwa kutumia lugha ya staha bila
matusi, sifa ya utekelezaji wa haraka apatapo matatizo ya Wananchi wake
pamoja na sifa ya kutetea demokrasia, uhuru na kutetea wanyonge.
“Faida
za shindano la tuzo hizi ni kwamba zinaweka Wananchi karibu na
viongozi, kuchochea utekelezaji huduma na maendeleo kwa kasi ya juu,
utawla bora na uwajibikaji wa viongozi kwa Wananchi, uhusiano mzuri kati
ya serikali na Wananchi na kuimarisha furaha, utulivu na amani,”
alieleza Maage.
Kwa
upande wake Mkurugenzi mkuu wa Kamati hiyo, Herman Mnenuka alisema kuwa
Wananchi ndiyo nguzo kuu ya kupata kiongozi atakayepata tuzo hiyo kwani
wao ndio watakaopendekeza majina ya wabunge pamoja na mawaziri wanaofaa
kuwania tuzo hiyo.
Katika
tuzo hiyo, hatua ya kwanza, wananchi wanapaswa kupendekeza wabunge 15
kwa kila kigezo shindanishi, pia Wananchi watawateua Mawaziri 5 kwa kila
kipengele shindanishi kwaajili ya kuingia kwenye ushindani wa tuzo hiyo
na wabunge watano na Mawaziri watatu watakaopata kura nyingi kwa njia
ya ujumbe mfupi (SMS) kutoka kwa wananchi wataingia katika fainali ya
king’anyiro kuwania tuzo hiyo.
Aidha
aliongeza kuwa, katika hatua nyingine, wananchi kupitia simu
watawachuja washiriki waliofika hatua ya fainali kwa kutuma SMS na
mbunge pamoja na waziri atakayepata kura nyingi ndiye atakaye kuwa
mshindi katika kilele cha tuzo hiyo kitakachofanyika tarehe 23 Desemba
Mwaka huu.
“Niwaombe
wananchi washiriki kikamilifu ili kuweza kupata kiongozi
anayejishughulisha na anayechapa kazi kupitia tuzo hii na mwisho wa
kilele tutapata mshindi wa kila kipengele kilichowekwa ambacho kina tija
muhimu katika taifa kupitia waheshimiwa wabunge na mawaziri wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,” alieleza Mnenuka.
Aidha
aliongeza kuwa, Wananchi watapendekeza majina kwa kutuma ujumbe mfupi
wa simu kupitia namba 15555 kwa mitandao ya Tigo, Airtel, Vodacom,
Halotel Smart na Zantel na kila SMS itatozwa gharama ya shilingi 500
vilevile kutakuwa na vipindi vya radio runinga na magazeti ili
kuwakumbusha mwenendo na hatua za shindano la tuzo za THSDA hadi siku ya
kilele.
Hizi
ni tuzo za kwanza kuandaliwa hapa nchini na kamati hiyo ambazo
zitafanyika kwa awamu kulingana na upatikanaji wa rasilimali fedha.
No comments:
Post a Comment