Maisha ya watoto
pacha waliozaliwa wakiwa wameshikana yako hatarini iwapo hawataondolewa
ukanda wa Gaza, kwa mujibu wa madaktari.
Alam Abu Hamna kutoka
hspitali ya Shifa, ilisema kuwa hali inayowakumba watoto hao wasichana
ni ngumu na kwamba haiwezi kutatuliwa na madaktari wa hospitali zilizo
ukanda wa Gaza.
Ilisema kuwa matumaini ni kuwa watoto hao watasafirishwa ng'ambo ili watenganishwe
Watoto hao walizaliwa Jumamosi na mmoja wao anatajwa kuwa dhaifu kuliko mwingine.
Hata hivyo kila mmoja ana moyo wake na mapavu. Mapacha ambao hutumia kiungo kimoja mara nyingi hukumbwa wna hatari ya kuishi.
"Maisha yao yako hatarini, ni hali iliyo ngumu," Dr Abu Hamna alinukuliwa akisema na gazeti la Times la Israel.
Alisema hali ya mmoja wa mapacha hao iko shwari la mwenzake yuko hali mbaya na anahitaji matibabu.
"Ikiwa watasafirishwa nje kwa haraka kupata matibabu nje, maisha yao yataokolewa," alisema.
Kitengo
cha jeshi la Israel kinachohusika na kuratibu kuingia na kuondoka
ukanda wa Gaza kinasema kuwa hakijapokea ombi lolote la mapacha
kuondolewa eneo hilo.
Mapacha waliozaliwa wakiwa wameshikana katika Ukanda wa Gaza mwezi Novemba mwaka 2016 baadaye walikufa.
Israeli
na Misri wameka vizuizi vya ardhini na baharinin kwa Ukanda wa Gaza
kwa miaka kumi katika jitihada za kuzuia mashambulizi kutoka kwa
wanamgambo.
No comments:
Post a Comment