Mahakama imeombwa kuingilia kati na kuamua -
iwapo uchaguzi wa marudio
utafanyika..
Wanataka uchaguzi huo uahirishwe.
Rais Uhuru Kenyatta anasema uchaguzi
utafanyika kama ulivyopangwa siku ya Alhamisi.
Muungano wa upinzani chini ya kinara Raila
Odinga umetaka wafuasi wake wasusie zoezi hilo, ukiutaja kuwa uchaguzi usioweza
kuwa wa huru na wa haki.
Odinga amesema Serikali ya Kenya na tume ya
Uchaguzi zimeshindwa kushughulikia mapungufu yaliyosababisha mahakama ya juu
zaidi nchini humo kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika
mwezi Agosti.
Hatua hiyo inajiri baada bya mahakama hiyo
kufanya uamuzi wa kihistoria ilipofutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais na
kutaka uchaguzi huo kurejelewa.
Kuna utata kati ya sheria za uchaguzi, katiba
na vile mahakama ilivyofafanua sheria hizo.
Mahakama ya juu imekubali kusikiliza ombi
hilo la muda wa lala salama ambalo linahoji iwapo tume ya uchaguzi na
mwenyekiti wake wataweza kufanya uchaguzi ulio huru na haki siku ya Alhamisi.
Kumeshuhudiwa maandamano ya wafuasi wa
upinzani wanaopinga uchaguzi huo wa marudio na wanashinikiza maguezi ndani ya
tume ya uchaguzi IEBC na pia katika mfumo wenyewe wa uchaguzi.
No comments:
Post a Comment