Rais
John Magufuli leo Oktoba 18, 2017 amemtumia ujumbe Mfalme wa Oman
Mtukufu Sayyid Qaboos bin Said Al Said na wawekezaji wengine wa Oman
kuwa atafurahi kuona wanakuja kuwezeka nchini tena kwa haraka na kudai
serikali itatoa ushirikiano.
Rais
ametuma ujumbe huo kwa mfalme wa Oman kupitia kwa Waziri wa Mafuta na
Gesi wa Oman Mhe. Dkt. Mohammed Hamad Al Rumhy
aliyeongozana na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salem Ben Nasser Al Ismaily na Naibu Waziri wa Utalii Mhe. Maitha Saif Majid, ambao walikua Ikulu Jijini Dar es Salaam.
aliyeongozana na Waziri wa Uwekezaji wa Oman Mhe. Salem Ben Nasser Al Ismaily na Naibu Waziri wa Utalii Mhe. Maitha Saif Majid, ambao walikua Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mfalme
wa Oman Mtukufu Sayyid Qaboos bin Said Al Said amemhakikishia Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa nchi
hiyo ipo tayari kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kwa
kuongeza uwekezaji katika viwanda, uzalishaji wa nishati, kuongeza
thamani ya madini, kuendeleza sekta ya gesi na mafuta na kuendeleza
ukanda wa uwekezaji wa Bagamoyo ili kukuza uchumi kwa kasi zaidi.
“Mhe.
Dkt. Mohamed naomba ukamwambie Mfalme kuwa namshukuru kwa ujumbe huu na
namkaribisha sana Tanzania, nimefurahi kuona mpo tayari kushirikiana
nasi kujenga viwanda, kuzalisha mazao na kuendeleza ukanda wa uwekezaji
wa Bagamoyo, sisi tupo tayari hata leo, njooni tushirikiane kwa sababu
nyinyi ni ndugu zetu na tutafanya uwekezaji kwa faida yetu sote” amesema
Mhe. Rais Magufuli.
Aidha,
Mhe. Rais Magufuli ametaka Oman iongeze ushirikiano na Tanzania katika
masuala ya utalii na usafiri wa anga, kuwekeza katika usindikaji wa
nyama na uvuvi na ushirikiano katika kubadilishana wataalamu wa nyanja
mbalimbali wakiwemo walimu wa lugha ya Kiswahili na Kiarabu.
Mbali
na hilo Rais Magufuli amemshukuru Mfalme wa Oman kwa msaada kujenga
visima vya maji 100 hapa nchini na amemuomba kuungana na Serikali katika
safari yake ya kuhamia Dodoma kwa kujenga miundombinu itakayoweka
kumbukumbu ya ushirikiano wa kidugu na kihistoria kati ya nchi hizi
mbili.
No comments:
Post a Comment