Watu saba wamefariki dunia katika ajali ya gari aina ya Scania
katika Mlima wa Kasagamba kijiji cha Mkongoro barabara ya kutoka
Manyovu wilaya ya Kigoma Vijijini kuelekea mkoani Kigoma.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma Maltini Otieno amesema
ajali hiyo imetokea leo Machi 21,2018 majira ya saa tatu asubuhi.
Amesema gari aina ya Scania lori yenye namba T741AAB ilianguka na
kusababisha vifo vya watu saba akiwemo dereva wa gari hiyo aliyefahamika
kwa jina la Siri Hamis (43) mwenyeji wa Singida pamoja na utingo wake
aliyefahamika kwa jina la Ramadhani Saidi (23) mkazi wa Manyoni.
Kamanda Otieno amesema katika gari hiyo walikuwa wamebeba mizigo na
watu wanne mmoja mwanamke na wa tatu wanaume ambapo wote walifariki na
majina yao hayakufahamika.
Aidha amesema ajali hiyo pia imesababisha kifo cha mwanafunzi
aliyefahamika kwa jina la Eliakimu Samsoni (15 )aliyekuwa akitembea kwa
miguu kuelekea shuleni na gari hilo kumgonga akiwa anatembea.
Amesema chanzo cha ajari hiyo ni dereva kushindwa kuimudu gari
kwenye mteremko mkali na kusababisha gari hiyo kutelemka kwa mwendo
mkali na kumshinda dereva huyo na kusababisha vifo hivyo.
Kamanda Otieno amewaomba madereva kuzingatia sheria za barabarani
na kuhakikisha gari za mizigo hazibebi abiria ili kunusuru vifo
vitokanavyo na ajali na kuhakikisha wanazingatia alama za barabarani.
Mabaki ya lori baada ya ajali – Picha na Rhoda Ezekiel – Malunde1 blog
No comments:
Post a Comment