Monday, March 12, 2018

Urusi yafanya jaribio la Kombola lisilozuilika.

Urusi imesema kuwa imefanikiwa kufanya jaribio la kombora lisiloweza kuzuilika ambalo ni miongoni mwa makombora yaliyotangazwa na Rais wa nchi hiyo, Vladmir Putin katika kampeni zake.

Wizara wa ulinzi ya Urusi imeonyesha video ambayo ilikuwa ikionyesha kombora hilo likifyatuliwa kutoka kwenye ndege ya kivita.

Kombora hilo liitwalo  Kinzhal limeelezwa kuwa linaweza kusafiri mara kumi ya kasi ya sauti na linaweza kufika hadi kilomita 2,000 ambapo pia  haliwezi kuonekana katika rada za kijeshi.

Hata hivyo, hatua hiyo ya jaribio la silaha hiyo ya nyuklia imefanyika ikiwa ni utekelezaji wa sera ya rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin ambaye anatarajiwa kuchaguliwa tena kuendelea kuiongoza nchi hiyo hivi karibuni.

Kama sehemu ya hotuba yake kwa taifa ya tarehe mosi mwezi hu, Putin alicheza kanda ya video ambayo ilionyesha  mvua ya makombora  yakitua katika jimbo la Florida nchini Marekani.

Marekani ilijibu ikisema tabia hiyo haikupaswa kufanywa na taifa kama Urusi

No comments:

Post a Comment