Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amewataka wanawake wote
waliotelekezwa na waume zao na hawapatiwi fedha za matunzo ya mtoto
wafike ofisini Jumatatu ya Aprili 9 kwa lengo la kupatiwa msaada wa
kisheria.
Taarifa
ya Makonda kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana amesema jopo la
wataalamu wa sheria, maofisa ustawi wa jamii na askari Polisi kutoka
dawati la jinsia wamejipanga ipasavyo kuwahudumia na kuhakikisha mzazi
mwenza anatoa fedha kwa ajili ya matunzo ya mtoto.
"Huduma
hii inatolewa bure chini ya uongozi thabiti wa Serikali ya Awamu ya
Tano.Ewe mwanamke huu si wakati wa kulia wala kuteseka kwani Serikali
yako itasimama na wewe hadi upate haki yako," amesema Makonda.
No comments:
Post a Comment