Thursday, March 15, 2018

SERIKALI YA SWEDEN YATOA BILIONI 66 KUKABARATI KITUO CHA KUZALISHIA UMEME CHA HALE HYDRO SYSTEMS WILAYANI KOROGWE


Serikali ya Sweden imetoa kiasi cha fedha Bilioni 66 za kitanzania sawa na  dola za Marekani milioni 30 ambazo zitatumika katika kukarabati mitambo katika Kituo cha Kuzalishia Umeme cha Hale Hydro System wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Hayo yamebainishwa na Balozi wa Sweden nchini Tanzania Katarina Rangnitt wakati alipotembelea mgodi huo ambapo upo Hale wilayani Korogwe Mkoani Tanga.

Amesema kuwa Tanzania na Sweden zina historia za muda mrefu katika uhusiano wa kidplomasia na nyanja mbalimbali za uchumi na kijamii.

Amesema kuwa nishati ni jambo muhimu kwa maendeleo ya viwanda hivyo kwa kuona umuhimu wa jambo hilo kwa nia moja serikali ya Sweden imetoa kiasi hicho cha fedha katika kukarabati mgodi huo.

upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella amemshukuru balozi huyo kwa serikali ya Sweden kufadhili mradi huo,pia amemkaribisha balozi huyo kuwekeza katika sekta mbalimbali za kijamii na uchumi.

Kwa upande wake Meneja wa Mtambo wa Uzalishaji Umeme wa Hale Mhandisi Steven Mahemba amesema kuwa mtambo huo umepunguza uzalishaji kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo uchakavu wa mitambo.


No comments:

Post a Comment